Chemundugwao: Ushindani umeongezeka | Mwanaspoti

NYOTA wa zamani wa Dar City, Trofimo Chemundugwao amesema mmiliki wa timu hiyo, Musa Mzenji ameufanya mchezo huo kuwa na ushindani mkubwa, kutokana na uwepo wa wachezaji nyota wa kimataifa kutoka nje ya nchi aliowaleta.

Trofimo ambaye kwa sasa yuko Iringa Kikazi, alisema uwepo wa wachezaji hao, umewafanya wachezaji wazawa waongeze juhudi zaidi uwanjani na kuleta ushindani.

Alisema mmliki huyo aliwahi kuwekeza Pazi iliyoshiriki mashindano ya ubingwa wa Afrika (BL) Afrika ya kusini na aliwasajili wachezaji wa kimataifa, Rucklin Louis [Morocco), Deing Dhieu (Sudan) anayeishi Marekani na Ndikumana Landry (Burundi).

Trofimo aliongeza, baada ya hapo aliianzisha Dar City mwaka 2023 na mwaka huu 2024, ikatwaa ubingwa wa Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), ikiwa na nyota wa kigeni kama Victor Mwoka, Marbuary Bramweli (Kenya) na Jamel Marbuary (Marekani)

Wakati huo huo FOX Divas ya Mara imeendelea kuonyesha ubora kwenye ligi ya kikapu ya taifa (BDL), baada ya kuifunga Vijana Queens kwa pointi 58-56, kwenye Uwanja wa Chinangali, Dodoma.

Mchezo huo ulionekana kama ni fainali kutokana na ushindani mkubwa uliokuwa unaonyeshwa kwa timu zote mbili ilishuhudiwa

Fox Divas ambao ni bingwa wa mkoa wa Mara, ikianza mchezo kwa uelewano kwa pasi fupi na ndefu na kuongoza kwa pointi 16-8.

Robo ya pili Fox Divas iliongoza tena kwa pointi 17-15 na hadi kufikia mapumziko ilikuwa mbele kwa pointi 33-23.

Hata hivyo, robo ya tatu Vijana Queens iliongoza kwa pointi 22-11, kabla ya robo ya nne Fox Divas kupata pointi 14-11.

Related Posts