RC Batilda awaomba waganga wa tiba asili kukabiliana na vitendo vya ukatili

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dkt. Batilda Burian, amekutana na viongozi wa Chama cha Waganga wa Tiba za Asili Tanzania wa Mkoa wa Tanga na kutoa wito wa kudhibiti vitendo ukatili wa kijinsia unaofanyika ndani ya jamii pamoja na kushiriki katika uchaguzi wa Serikali na kuepuka ramli chonganishi .

Akizungumza katika mkutano huo, Dkt. Batilda ameeleza kuwa”vitendo vya ukatili wa kijinsia vimekuwa vikiongezeka na kuathiri jamii,  ninasisitiza  kuwa waganga wa jadi wana nafasi muhimu katika jamii, hivyo ni wajibu wenu kutumia ushawishi mlionao katika kuhamasisha maadili mema na kuelimisha wananchi juu ya haki na usawa wa kijinsia”

Mwenyekiti wa Chama cha Waganga wa Tiba za Asili Tanzania Seleman Iddy kwa upande wake, ameahidi kuwa
“chama hiki kitashirikiana na Serikali kwa karibu ili kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia na waganga wa jadi wamejipanga kuhakikisha kuwa wanalinda haki za binadamu na kuondoa mila na desturi zinazochangia unyanyasaji wa kijinsia”

Pia waganga wa tiba asili Mkoa wa Tanga wameeleza wasiwasi wao juu ya kuibuka kwa vyama visivyo rasmi vya waganga ambavyo vinajihusisha na utapeli kwa wananchi, na wametoa wito kwa serikali kuchukua hatua kali dhidi ya vyama hivo na kuhakikisha kuwa vyama vinavyosajiliwa vinafuata taratibu na kanuni za tiba asili ili kulinda heshima na imani ya wananchi kwa tiba hizo.

“Kiukweli mhe.mkuu wa Mkoa hivi Sasa Kuna matapeli na siyo waganga inatuharibia sana ambao waganga tulio wakweli kila mtu akiibuka huko anasema ni Mganga wakati siyo kweli ndiyo hao wanafanya mambo ambayo si ya kweli
amesema “Juma Kaoneka Katibu Mkuu – (CHAWATIATA TANGA)

Related Posts