Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda alivyowasili Bungeni jijini Dodoma tayari kuwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Bajeti ya Wizara ya Elimu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 ina kauli mbiu inayosema ‘Elimu ujuzi ndio mwelekeo’ ikiwa na maana msisitizo na mkazo katika mitaala yetu utajikita zaidi katika kuhakikisha wahitimu wanakuwa na ujuzi utakaowawezesha kujiajiri na kuajiri wengine.