BoT Yatoa Mafunzo kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu Mikopo ya Mtandaoni

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari mkoani Dar es Salaam kuhusu mikopo ya mtandaoni, lengo likiwa ni kuongeza ufahamu wa jamii kuhusu masuala yanayohusu mikopo hiyo.

Akizungumza wakati akifungua Mafunzo hayo leo Novemba 14, 2024 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Huduma Ndogo za Fedha, Dickson Gama amesema BoT itaendelea kuhakikisha sekta ya fedha inakuwa thabiti, imara na stahimilivu ili kuwawezesha  shughuli za uchumi zinapatikana kwa wakati.

“Ni jukumu la BoT katika kusimamia huduma Ndogo za fedha nchini  hivyo kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya habari kiunganishi kati  ya Benki Kuu na jamii ya watanzania  na dunia kwa ujumla,”Amesema

Ameeleza kuwa mikopo ya mitandaoni imekuwa ni sehemu  ya mfumo wa fedha kwani imerahisisha utoaji  wa huduma za mikopo kwa urahisi zaidi  na haraka. 

Amesema ukuaji huo wa haraka umesababisha changamoto  kadhaa ikiwemo  masuala  ya kimaadili, riba kubwa gharama kubwa za mikopo na kukosekana kwa taarifa. 

Pamoja na hayo amesema kutokana na changamoto hizo wamekuwa mstari wa mbele kutoa elimu ili kufanya huduma hiyo kuwa na manufaa kwa wananchi  na mtoa  huduma  kuidhinishwa na BoT.












Related Posts