Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amemueleza Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomiki IAEA Rafael Grossi, kwamba serikali yake iko tayari kutatua masuala yenye utata kuhusu mpango wake wa atomiki, kabla ya Donald Trump aingie madarakani.
Grossi aliyekuwa ziarani mjini Tehranjana, alisema kwamba mazungumzo ya tija kuhusu nyuklia na Iran ni muhimu ili kuepusha mzozo mpya katika eneo ambalo tayari limegubikwa na vita vya Israel dhidi ya Hamas na Hezbollah. Akiwa mjini Tehran, Grossi alisema mitambo ya nyuklia ya Iran “haipaswi kushambuliwa.”
Ziara yake inafanyika siku chache baada ya waziri mpya wa ulinzi wa Israel, Israel Katz kusema Iran iko hatarini zaidi kuliko hapo awali.Shirika la IAEA limeitaka Iran kushirikiana haraka na kikamilifu
Pezeshkian alimwambia Grossi kwamba “kwa kuwa tumethibitisha mara kwa mara nia yetu njema, tunatangaza utayari wetu wa kushirikiana na kuungana na shirika hili la kimataifa kutatua utata unaodaiwa kuwepo na mashaka juu ya shughuli ya amani ya nyuklia ya nchi yetu.” Iran yasema mazungumzo na mkuu wa IAEA yalikuwa mazuri
Kuna wasiwasi kwamba Trump aliye na msimamo mkali dhidi ya Iran huenda akaipatia Israel nafasi huru zaidi baada ya kuchukua madaraka mwezi Januari.
Waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi, ambaye pia alikutana na Grossi, alisema Iran ilikuwa “tayari kufanya mazungumzo” kwa kuzingatia “maslahi ya kitaifa” na “haki zisizoweza kuepukika,” lakini haiko “tayari kufanya majadiliano chini ya vitisho na shinikizo”.
Araghchi alikuwa mpatanishi mkuu wa Iran katika mazungumzo ambayo yalipelekea makubaliano ya kihistoria ya nyuklia ya 2015 na mataifa makubwa, ambayo Trump alijiondoa miaka mitatu baadaye.
Grossi pia alikutana na mkuu wa shirika la nishati ya atomiki la Iran, Mohammad Eslami. Eslami aliuambia mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari kwamba Iran itachukua “hatua za mara moja” dhidi ya vikwazo vyovyote kutoka kwa bodi ya magavana wa IAEA.
Ameongeza kuwa “azimio lolote la uingiliaji kati katika masuala ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran bila shaka litakabiliwa na hatua za mara moja,” alisema Eslami. Ziara ya Grossi ni ya pili mjini Tehran mwaka huu lakini ni ya kwanza tangu kuchaguliwa tena kwa Trump.
Wakati wa muhula wake wa kwanza katika Ikulu ya White House kutoka 2017 hadi 2021, Trump alipitisha sera inayoitwa “shinikizo la juu” ambayo ilirejesha vikwazo vya kiuchumi vya Washington dhidi ya Iran ambavyo awali viliondolewa chini ya makubaliano ya 2015.Iran yaridhia IAEA kuendelea kukagua vituo vya nyuklia
Katika kushughulikia vikwazo hivyo, Iran ilianza kurudi nyuma katika utekelezaji wa ahadi zake chini ya mpango huo, ambao uliizuia urutubishaji uranium kwa zaidi ya asilimia 3.65.