Utengenezaji wa mabehewa 264 ya mizigo umekamilika nchini China -TRC

Shirika la Reli Tanzania – TRC limesema utengenezaji wa mabehewa 264 ya mizigo umekamilika nchini China.

Meli iliyobeba mabehewa hayo imeng’oa nanga nchini China Novemba 12, 2024 na inatarajiwa kufika Tanzania katikati ya mwezi Disemba 2024.

Katika mzigo huo kuna mabehewa 200 ya kubeba makasha (makontena) na mabehewa 64 ya kubeba mizigo isiyofungwa (loose cargoes).

Shehena hiyo ya mabehewa 264 ni sehemu ya jumla ya mabehewa 1,430 ambayo kwa mujibu wa mkataba yanatakiwa kutengenezwa na kampuni ya CRRC.

TRC inategemea kuanza kusafirisha mizigo kwa reli ya SGR kati ya January au February mwakani

Related Posts