Mike Tyson Vs Jake Paul mpambano ni leo,mpinzani atamba ‘nitamuua’

Mike Tyson yuko tayari kurejea kwenye ulingo wa ndondi huku atakapomenyana na bondia aliyegeuka kuwa YouTuber, Jake Paul kwenye Uwanja wa AT&T mjini Arlington, Texas.

Pambano hilo limepangwa kufanyika leo usiku kulingana na muda wa Marekani na linaweza kutiririshwa moja kwa moja

Wawili hao tayari wamekuwa na majibizano mengi kwenye mitandao ya kijamii katika mkutano wa waandishi wa habari lakini hali ya mwisho ya wawili hao kuchuana ilichukua mkondo mbaya, na kuongeza joto zaidi katika pambano hilo lililotarajiwa.

Wakati wa upimaji huo rasmi, ambao ni utaratibu wa kimila kabla ya pambano zote za ndondi, Tyson alishindwa kuzuia hisia na kumpiga konde la shavu Paul kwa mkono wake wa kulia.

Tukio hilo lilianza baada ya Paul kuonekana akimdhihaki Tyson na walinzi waliokuwepo walianza kuwatenganisha wawili hao kabla mambo hayajawa mabaya zaidi.

Pambano linalosubiriwa kwa hamu kati ya bondia nguli Mike Tyson na MwanaYouTube Jake Paul

 

Related Posts