Serikali itaendelea kuwawezesha Wajasirimali Wanawake na Vijana

 

 

Na. Mwandishi wetu – Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema serikali itaendelea kuwawezesha Wajasiriamali Wanawake na Vijana kwa kuwapatia maarifa, masoko, fursa za kijamii na kiuchumi ili waweze kupiga hatua katika kujenga uchumi wa familia na jamii kwa ujumla.

Aidha, amesema   Wajasiriamali Wanawake ni nguzo muhimu katika kutengeneza Ajira na kukuza uchumi wa maendeleo ya Taifa, hivyo uwekezaji kwao ni kipaumbele cha serikali katika kuhakikisha wanapata nafasi sawa.

Mhe. Ridhiwani amebainisha hayo leo Novemba 13, 2024 Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya Panda event 2024, ambayo ilikuwa na kauli mbiu isemayo Wawezeshe Wasichana na Wajasiliamali kuvumbua fursa za masoko na kuboresha viwanda

Amesema Serikali imejipanga kutoa sera zinazohimiza uwezeshaji wa kifedha, programu zinazojenga daraja la kidijitali na kuhimiza ushirikiano wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wanawake.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Panda event, Irene Matunda, amesema lengo la pande event ni kuvunja duara la umasikini na kuwaunganisha vijana kiuchumi kwa kutumia mbinu za uwezeshaji kiuchumi na teknolojia kwa kutoa ujuzi wa uzalishaji biashara.

 

Related Posts