DKT. PHILIP MPANGO MGENI RASMI, KONGAMANO LA TATU LA KIMATAIFA LA KISAYANSI LA TAFORI

NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Philip Mpango anatarajia kuwa mgeni rasmi kongamano la kimataifa la tatu ,kisayansi litakalofanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 11hadi 13 December mwaka huu lenye lengo la kujadiki juu ya kurudisha madhari ya misitu kwa maendeleo endelevu na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Kongamano hilo litafanyika kwa siku tatu, kuanzia Disemba 11 hadi 13, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha, (AICC) mada kuu katika kongomano hilo ni Kurejesha Mandhari ya Misitu kwa Maendeleo Endelevu na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchiā€ yaani (Restoring Forest Landscapes for Sustainable Development and Climate Change Mitigation).

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania Dkt. Revocatus Mushumbusi amesema kuwa kongamano hilo linatarajiwa kuwakutanisha wadau zaidi ya 400 kutoka ndani na nje ya nchi, wanasayansi,watunga sera,wanazingira, vyuo vikiuu ,wapanda miti pamoja na wadau wengine.

Amesema lengo kuu la kongamano hilo ni kuwakutanisha wataalam kutoka katika sekta ya misitu ya wafugaji nyuki kujadiliana kwa pamoja na kubadilishana uzoefu juu ya usimamizi wa maliasili misitu na nyuki.

Kupitia kongamano hilo, wataalamu wa ndani na nje wataweza kutumia nafasi kutoa matokeo ya tafiti zilizofanyika na kuibua miradi mipya ya uhifadhi kwa lengo la Kurejesha na Kuongoa Misitu kwa Maendeleo Endelevu na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.

Amsema Kongamano hilo litakuwa ni sehemu ya kuchochea na kuhamasisha wadau kushirikiana na Serikali kwenye maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wafugaji Nyuki Duniani (APIMONDIA) unaotarajiwa kufanyika nchini mwaka 2027.

Aidha Dk. Mushumbusi amewataka wadau wa sekta ya Misitu na ufugaji Nyuki kushiriki katika kongamano hilo kwa kufanya usajili kupitia Tovuti ya Taasisi www.tafori.or.tz

kwa kulipia kiingilio cha Tsh. 200,000 kwa Wadau wa Afrika Mashariki. Tsh 100,000 Wanafunzi na Tsh. 350,000 kwa wadau wa nje ya Afrika Mashariki.

Related Posts