WAZIRI MKUU AONGOZA MAZIKO YA MAREHEMU LAWRENCE MAFURU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 15, 2024 ameungana na ndugu, jamaa, marafiki na viongozi wengine wa Serikali katika mazishi ya aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Tume ya Mipango, Marehemu Lawrence Nyasebwa Mafuru.

Maziko hayo yamefanyika katika Makaburi ya Kondo, Ununio jijini Dar es Salaam.

Marehemu Mafuru alifariki Novemba 09, 2024 katika Hospitali ya Apollo nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.



Related Posts