Ramovic: Timu yangu sitaki ulevi, pati

Wakati Yanga ikimtambulisha kocha mpya, Sead Ramovic, wachezaji wa timu hiyo wametakiwa kujiandaa kisaikolojia kwani hataki sterehe zikiwemo ulevi na kujirusha.

Ramovic ambaye ni kocha wa zamani wa TS Galaxy ya Afrika Kusini, alishusha mkwara huo wakati akitua kwenye klabu hiyo siku chache baada ya kusaini mkataba Oktoba Mosi, 2021.

Alitangaza mbele ya waandishi wa habari namna ya kusimamia nidhamu, ambapo alisema kwenye timu yake hataki kuona wachezaji wanajikita kwenye ulevi au kufanya sherehe.

“Narudia… Kwenye timu yangu sihitaji ulevi wala kufanya sherehe, wala mienendo isiyofaa, sijali na kama unataka kufanya utakuwa nje ya hii timu,” alisema Ramovic kwenye utambulisho huo huku akiongeza:

“Kwa sababu kama unataka kupiga hatua, kama unataka mafanikio tunahitaji wachezaji wanaojitambua. Kwa kuwa muda wa kucheza soka ni mfupi, huwezi kucheza kwa miaka 50, utacheza kwa miaka 10 au minane utakuwa na bahati sana ukicheza kwa miaka 15.”

Kauli hiyo ya Ramovic itakuwa mwiba kwa wachezaji wa Yanga iwapo watakwenda kinyume na utaratibu wa kocha huyo.

Related Posts