ZISA Yajipambamua kwa Wanachama wake kuondokana na Mikopo ya Kausha damu.

 

Na Jane Edward, Arusha 

CHAMA cha Zimamoto Saccos (ZISA) kimefanya mkutano mkuu wa sita wa chama hicho ambapo wanachama wameweza kutoa michango yao namna chama kinavyotakiwa kuwa na pia kusomewa taarifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na taarifa za mapato na matumizi pamoja na hali ya kifedha ya chama .
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Arusha,Mlezi wa Zimamoto SACCOS (ZISA) ambaye pia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Tanzania,John Masunga, katika kikao  kilichowashirikisha wanachama wa chama hicho.

Masunga amesema kuwa,chama hicho ni chama cha ushirika kipya na kilianzishwa mwaka 2018 ambapo katika kipindi kifupi kimekuwa na mafanikio makubwa ambapo kimeongeza wanachama wengi kwa muda mfupi. 
Amesema kuwa,katika kipindi kifupi tangu chama hicho kianzishwe kina takribani wanachama zaidi ya elfu moja na bado ongezeko la wanachama ni kubwa na askari wamepata elimu na wameelimishwa juu ya saccos na wanazidi kujiunga kwa wingi . 
Naye Mwenyekiti wa bodi ya Zimamoto Saccos Ltd,Elisa Mugisha amesema kuwa,chama bado ni kichanga na wanafanya vikao vyao kwa ufanisi mkubwa sana .
Amesema kuwa kauli.mbiu ya chama hicho ni “Wekeza sasa ushirika ni maisha “,hivyo askari wa jeshi la Zimamoto na uokoaji na watumishi wengine kwa ujumla wamekuwa wakiwekeza kwenye chama hicho cha akiba na mikopo na wamekuwa wakipata mikopo ya riba nafuu sana na kufanya maswala mbalimbali ya maendeleo. 
Amesema kuwa, wanatoa mkopo hadi wa milioni 30 lakini kwa riba ya asilimia moja kwa mwezi na hivyo wanatoa riba ndogo ili watu.wengi wanufaike kuliko kuweka riba kubwa .
“Ukiacha mikopo kwa ajili ya kujenga nyumba pia kuna mikopo kwa ajili ya kujiendeleza kielimu na hata kuna mkopo wa dharura ambapo unaweza kupata hadi milioni nne na kurejesha vizuri kwa utaratibu mzuri ambapo pia ukitaka kuchukua likizo kama hela yako ya likizo haijatoka kwa mwajiri unaweza kuchukua mkopo wa likizo na utarejesha ukirudi .alisema Mugisha.
“Tunamshukuru sana mlezi wetu kwani amekuwa akitoa mchango mkubwa sana kwenye chama kwa hiyo ile faida kidogo tunayopata tunarudisha mle na hivyo tunapata faida kubwa kwa muda mfupi.”alisema .

 

Related Posts