Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema hadi sasa mtu mmoja pekee amefariki dunia, huku wengine 28 wakijeruhiwa katika ajali ya jengo la ghorofa lililoporomoka eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Novemba 16, 2024.
“Uzuri tumeambiwa ndugu wanaendelea kupata mawasilianao na ndugu zao waliopo hapo chini na uzuri nimeona nikiwa hapa mmoja aliyeokolewa amesema wenzangu wapo chini, kwa hiyo kazi inaendelea ya kuwaokoa waliopo chini na nataka tuhakikishe hapa hatutumii nguvu tutatumia akili zaidi,” amesema Majaliwa.
Mpaka sasa shughuli za uokoaji zinaendelea katika eneo hilo, huku viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwa wamefika eneo hilo kwa ajili ya uratibu wa uokoaji.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa pole kutokana na ajali hiyo, huku akiagiza nguvu ya uokoaji iongezwe ili kunusuru maisha ya waathirika wa ajali hiyo.
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi