IGP WAMBURA AWAHAKIKISHIA WANANCHI HALI YA USALAMA KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

NOVEMBA 15,2024 KIDATU, MOROGORO

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura amewakumbusha wananchi kutekeleza haki yao ya kikatiba kwa kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali ya mitaa tarehe 27 Novemba 2024 na kwamba Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vimejipanga vyema kuhakikisha kwamba amani na utulivu vinatamalaki wakati wote kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

IGP Wambura ameyasema hayo Novemba 15,2024 wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo ya uongozi mdogo kwa Cheo cha Sajini Meja wa Polisi na Sajini Taji wa Polisi kozi namba 1/2024/2025 katika Chuo cha Maafisa wa Polisi Tanzania kilichopo Kidatu mkoani Morogoro.

Related Posts