Aussems ajihami mapema | Mwanaspoti

KOCHA wa Singida Black Stars, Patrick Aussems, baada ya kuuona moto wa wapinzani wake wa mchezo ujao Tabora United, amejihami mapema kuomba mechi ya kirafiki kukipima kikosi chake.

Singida itakayokuwa ugenini Novemba 24 mwaka huu kucheza mechi ya ligi dhidi ya Tabora United, leo Jumapili itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Fountain Gate ikiwa ni ombi la kocha huyo.

Ofisa Habari wa Singida Black Stars, Hussein Masanza, amesema: “Jumapili hii tutashuka katika Dimba la Tanzanite Kwaraa kucheza mechi ya kirafiki na majirani zetu Fountain Gate FC.

“Mchezo huu ni sehemu ya kujipima nguvu baada ya ligi kusimama huku tukiwa na mchezo mgumu mbele yetu dhidi ya Tabora United ugenini.”

Singida iliyotoka kupata suluhu na Coastal Union katika mchezo wa mwisho wa ligi kucheza, inakwenda kukabiliana na Tabora United iliyoichapa Yanga mabao 3-1.

Chini ya Kocha mpya raia wa DR Congo, Anicet Kiazayidi, Tabora United imeshinda mechi zote mbili alizosimamia dhidi ya Mashujaa na Yanga.

Related Posts