MSD YAKABIDHI DAWA NA VIFAA VYA DHARURA KUSAIDIA WAATHIRIKA WA AJALI KARIAKOO

Serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) imekabidhi baadhi ya dawa na vifaa vya dharura kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa ajali ya kuangukiwa na ghorofa Kariakoo, Dar es Salaam.

Vifaa hivyo vya dharura vilivyokabidhiwa kwa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Dkt. Zaituni Hamza ni pamoja na barakoa za aina N95, Surgical mask, vifaa vya magari ya dharura (Ambulance stretcher 15), mipira mbalimbali ya mikono, (Gloves) dawa za maumivu za vidonge na sindano, maji ya dripu, dawa za vidonda, pamba na gauze kwa ajili ya kufungia vidonda.

MSD inaendelea kushirikiana na timu ya dharura na maafa kwa kupeleka dawa na vifaa tiba vya dharura ili kusaidia waarhirika wa ajali



Related Posts