WAZIRI KOMBO AWASILI NCHINI ZIMBABWE KUHUDHURIA MKUTANO WA DHARURA WA SADC

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mhe .Balozi Mahmoud Thabit Kombo amewasili Harare, Zimbabwe,
tarehe 16 Novemba, 2024 kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Mawaziri wa
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ambao unatarajiwa
kufanyika tarehe 17 – 19 November 2024.

Waziri Kombo amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. IGP Mstaafu Simon Sirro.

Pia,
Mhe. Kombo amekutana na Ujumbe wa Tanzania unaoshiriki mkutano huo na
kupokea taarifa ya maandalizi ya mkutano huo ambao unalenga kujadili
masuala mbalimbali yanayohusu kanda hiyo hususan hali ya Ulinzi, Usalama
na mikakati ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba kanda.

Aidha mkutano huo utatanguliwa na mkutano wa Kamati ya Makatibu wakuu wa SADC utakaofanyika tarehe 17 November 2024.

Related Posts