Msimamizi wa uchaguzi Geita ateta na viongozi wa dini na makundi mbalimbali halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo

Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Shauri Selenda ametoa wito kwa viongozi wa Dini na makundi mbalimbali kwenye jamii kuhakikisha wanahamasiha wananchi kujitokeza na Kwenda kupiga kura siku ya tarehe 27 November 2024

Hayo ameyazungumza wakati alipokutana na makundi hayo katika ukumbi wa mikutano wa Halmshauri hiyo tarehe 15 November 2024 akiwa Pamoja na maafisa wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Halmashauri

Msimamizi huyo wa Uchaguzi Shauri Selenda amesema kuwa lengo la kukutana na makundi hayo ni kuzungumzia uchaguzi wa Serikali za Mita na kuwakumbusha ili waweze kusaidia kuzungumza na waumini wao waweze kujitokeza kupiga kura.

Pia katika upande mwingine Ndg Shauri amesema kuwa kwa upande wa maandalizi tayari wamekwishakamilisha maandalizi yote na wapo tayari kwa ajili ya uchaguzi na kuendelea kuwaasa wananchi wote wa Wilaya ya Bagamoyo kuhakikisha wanaenda kupiga kura siku hiyo ya tarehe 27 November 2024.

Pia Msimamizi wa Uchaguzi ametoa rai kwa upande wa wagombea kufanya kampeni zao kwa amani na usalama pindi itakapofika tarehe ya kuanza kwa kampeni hizo ambazo zitarajia kuanza tarehe 20 hadi 26 November mwaka huu

Kwa upande wa Mwakilishi wa Baraza la Amani Shekhe Hashimu Juma amesema kuwa jukumu lao la kwanza ni kuhakikisha wanapeleka elimu kwa waumini wao juu ya umuhimu wa amani huku pia wakiwaasa waumini hao kujitokeza Kwenda kupiga kura siku hiyo ya tarehe 27 November mwaka huu.

Mbali na yote hayo Viongozi hao wa dini walipata nafasi ya kufanya maombi ya kuombea Amani ya Taifa Pamoja na kuendelea kuwepo kwa amani katika kipindi chote cha uchaguzi na kuwaombea wasimamizi wote wa uchaguzi Kutenda haki kwa kila mgombea.

  

Related Posts