Geita. Mtu mmoja ambae jina lake halijafahamika amepoteza maisha na wengine 10 kujeruhiwa katika ajali ya iliyohusisha gari dogo na basi la abiria.
Ajali hiyo imetokea saa 3 usiku wa kuamkia leo, Novemba 17, 2024 katika eneo la Mpovu Barabara kuu ya Geita-Kagera ikihusisha gari dogo aina ya Kluger na basi dogo la abiria aina ya Tata.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mji wa Geita, Thomas Mafuru akizungumza na Mwananchi leo Jumapili amesema wamepokea majeruhi 10 na mwili mmoja wa jinsia ya kiume.
Amesema majeruhi wawili wamehamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Geita kutokana na hali zao kuwa mbaya, wakijeruhiwa zaidi maeneo ya miguu na tumbo.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi, Edwad Lukuba amesema ajali hiyo ilihusisha gari dogo aina ya Kluger likiendeshwa na mfanyabiashara wa madini ya dhahabu pamoja na gari la abiria likitokea Geita kwenda Katoro kugongana uso kwa uso.
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi…