Singano anakiwasha Mexico | Mwanaspoti

KLABU ya FC Juarez imetoa takwimu za nyota wa Tanzania, Julietha Singano kuwa mchezaji aliyepora mipira mingi zaidi Ligi Kuu ya Wanawake nchini Mexico.

Huu ni msimu wa tatu kwa Singano kucheza Ligi hiyo kubwa nchini Mexico tangu alipojiunga nao mwaka 2022/23.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa timu hiyo uliposti kwa msimu uliopita Singano ndio alikuwa mchezaji aliyepora mipira mingi zaidi ya hatari (57).

Ndani ya msimu huo kwenye mipira hiyo ya hatari aliyoitoa aliisaidia Juarez kumaliza nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi ikilingana na Pachuca iliyomaliza nafasi ya sita.

Hata hivyo licha ya rekodi hiyo ndiye mtanzania pekee ambaye ukiachana na Enekia Lunyamila wa Mazaltan na tangu ajiunge na timu hiyo amekuwa tegemezi eneo la ulinzi la Juarez.

Sio jambo rahisi kwa nyota huyo kucheza mbele ya wachezaji wa kimataifa akiwaweka nje na kuaminiwa na kocha huyo akianza na kucheza kwa dakika zote 90 kwenye kila mchezo.

Related Posts