WAZIRI KIJAJI ASHIRIKI MKUTANO WA MAWAZIRI WA MAZINGIRA COP29

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akishiriki Mkutano wa Mashauriano wa Mawaziri wa Mazingira wa Afrika (AMCEN) leo Novemba 17, 2024 ambapo umefanyika pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa (COP29) unaoendelea jijini Baku, Azerbaijan. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Kanizio Manyika.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Lujemeja (nyuma kushoto) na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Kemilembe Mutasa wakishiriki Mkutano wa Mashauriano wa Mawaziri wa Mazingira wa Afrika (AMCEN) leo Novemba 17, 2024 ambapo umefanyika pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa (COP29) unaoendelea jijini Baku, Azerbaijan.

Mawaziri wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Mkutano wa Mashauriano wa Mawaziri wa Mazingira wa Afrika (AMCEN) leo Novemba 17, 2024 ambapo umefanyika pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa (COP29) unaoendelea jijini Baku, Azerbaijan.

……

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ameshiriki Mkutano wa Mashauriano wa Mawaziri wa Mazingira wa Afrika (AMCEN) leo Novemba 17, 2024. 

Mkutano huo ni wa pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa (COP29) unaoendelea jijini Baku, Azerbaijan. 

Katika mkutano huo mawaziri wamejadili masuala ya mazingira pamoja na upatikanaji wa fedha za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. 

Pia, Mkutano wa Mawaziri wa Mazingira ni sehemu ya mkakati wa kuweka msimamo wa pamoja wa nchi za Afrika kwenye majadiliano yanayoendelea kwenye COP29. 

Tanzania imewakilishwa na Waziri Mhe. Dkt. Kijaji ameambatana na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Lujemeja na wataalamu.

Related Posts