Aliyekuwa kocha wa Yanga na sasa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusinu, Nasredine Nabi ametuma salamu za pole kwa waathirika walioporokewa na jengo Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Kocha huyo ametumia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika “ Pole sana kwa wananchi wa Tanzania, Mungu awe pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu” akimbatanisha na picha ya jengo la Kariakoo lililoporomoka.
Jengo hili liliporomoka jana asubuhi Novemba 16, 2024 ambapo hadi sasa vifo 13 vimeipotiwa na majeruhi 84.
Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuongoza timu ya wataalamu wa ujenzi kukagua majengo yote ya Kariakoo na kumpa taarifa, huku akilitaka Jeshi la Polisi kupata taarifa ya kina kutoka kwa mmiliki wa jengo hilo na jinsi ujenzi ulivyokuwa.