Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepongeza Taasisi ya Mafunzo ya Sayansi za afya Haydom kwa utoaji huduma za afya ikiwa ni jitihada za kuunga Mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwapatia huduma bora za afya watanzania.
Hayo yamesemwa mbele ya waumini wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Mbulu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Mizengo Pinda (Mb.) akimwakilisha Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha. Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba kwenye Sherehe ya Maadhimisho ya Miaka 40 ya Taasisi hiyo iliyopo Wilayani Mbulu Mkoani Manyara.
“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imatambua mchango wa kanisa katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuwapatia wananchi huduma bora” amesema Mhe. Pinda
Aidha Mhe. Pinda amewaasa wanafunzi wa Taasisi hiyo kutumia vema elimu wanayoipokea kwa kuendelea kujifunza kwa moyo wa kujitoa ili kuongeza ubunifu na kuondoa changamoto zinazoikabili sekta ya Afya hapa nchini.
“Nawaasa wanafunzi na wahitimu wa Taasisi hii Kuendelea kuwa na ari ya kujifunza, ubunifu na kujitolea katika Kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya afya” amesema Mhe. Pinda
“Muitumie Elimu na Ujuzi mliyonayo katika kuboresha maisha ya watu” ameongeza mhe. Pinda
Naye Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Mbulu John Nade ameishukuru Serikali ya awamu wa sita kwa kuiongezea taasisi hiyo nafasi za udahili wa wa wanafunzi kwa mwaka wa Masomo 2024/25 na 2025/26
“Tunaishukuru sana Serikali ya Jamhuri Muungano wa Tanzania kupitia ofisi ya rais Tamisemi kwa uamuzi wake wa kuipa taasisi hii wanafunzi 60 kwa mwako 24/25 na Wanafunzi 40 kwa mwaka 2025/26 kwa fani ya Radiolojia” ameseme John Nade Msaidizi wa Askofu.
Kwa Upande Wake Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe.. Fratei Gregory Massay amepongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kuleta watumishi kwa ajili ya kutoa huduma katika Taaasisi Hiyo.
“Niishukuru Serikali hasa Rais wetu wa Tanzania Mama yetu Dkt. Samia Suluhu hassan ameshatusaidia watumishi watano mpaka sasa na sio hapa tu hata hosptali yetu pia ametuletea” amesema Mhe. Fratei Mbunge wa Jimbo mbulu Vijijini.
Taasisi hii ilianzishwa kwa lengo la kusaidia kujenga uwezo wa kitaaluma na kutoa mafunzo bora katika nyanja mbalimbali za Sayansi za afya na kuchangia kuboresha huduma za afya ndani na nje ya nchi.