Waziri Mkuu aagiza Niffer ahojiwe na Polisi kwa kuchangisha fedha

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza mwanamitandao na mfanyabiashara, Jenifer Jovin ‘Niffer’ ahojiwe na Jeshi la Polisi, kwa kukusanya fedha za michango kwa ajili ya waathirika walioporomokewa na jengo la ghorofa.

Majaliwa ametoa amri hiyo leo Novemba 18, 2024 wakati akitoa katazo kwa watu mitandaoni kuchangisha fedha kwa ajili ya waathirika hao, huku akitaka Niffer akamatwe, akajibiwa kuwa ameshakamatwa.

“Tumeona kuna watu wameanza kuchangisha huko pembeni wanasema michango kwa ajili ya waathirika wa Kariakoo hapana, Serikali imeendelea kupokea kutoka kwa watu wema wakileta misaada yao hapa na walichokuwa wakileta ni maji. Sijaruhusu mtu yeyote huko nje aanze kuchangisha kwa ajili ya tatizo hili na hatukufanya hivyo kwa sababu kamati ya maafa ipo.”

“Huyo binti anaitwa Niffer nimeona anachangisha na anasema mpaka jana amechangisha zaidi ya Sh37 milioni, atafutwe kwanza atuambie nani alimpa kibali cha kuchangisha umma utaratibu huo anaotumia wa kuingiza pesa kwenye simu yake amepata kibali wapi na amekusanya shilingi ngapi. Anasema amenunua maziwa amepeleka wapi kwa kuwa Jeshi la Polisi mmeshampata mumuhoji mfunge hiyo akaunti na kupitia tangazo hili haturuhusu mtu mwingine yeyote kusimamia michango ya watu,” amesema Majaliwa.

Related Posts