EABC na TCCIA wakubaliana kukuza ujasiriamali kwa vijana Tanzania

Tanzania Chamber Of Commerce, Industry and Agriculture (TCCIA) na East Africa Business Consortium (EABC) leotarehe 18 Novemba 2024, wameingia kwenye makubaliano yaushirikiano (MOU) ili kukuza Ujasiriamali nchini Tanzania hususani kwa vijana.

TCCIA ikiwa ni taasisi yenye zaidi miaka 30 Nchini Tanzania inafanya kazi zake kwenye mikoa 26 na wilaya 150 NchiniTanzania. TCCIA imekua mbia mkubwa wa uendelezaji wabiashara, viwanda na kilimo nchini Tanzania. Kwa upandewake EABC ni taasisi iliyojikita katika kuendelezaUjasiriamali, Utalii, Ubunifu na miradi ya kukuza ajira kwavijana.

Makubaliano haya yanalenga kutumia uzoefu wa taasisi hizimbili kuleta maendeleo makubwa katika kukuza ujasiriamalinchini Tanzania hususani kwa vijana. Takwimu zinaonyeshaZaidi ya asilimia 80% ya Watanzania ni Vijana chini ya miaka40. Moja ya changamoto kubwa wanazopata vijana ni ukosefuwa ajira, hivyo ushirikiano wa TCCIA na EABC unalengakukuza ujasiriamali kama njia ya kukuza ajira nchiniTanzania. Kupitia makubaliano haya taasisi hizi mbilizitashirikiana katika kuendesha mafunzo na mikakati mingineya kukuza ujasiriamali nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Afisa Mtendaji Mkuu waEABC Imani Kajula alisema ‘’ Tanzania ni moja kati ya Nchi43 zilizokubali kuanzishwa kwa soko huru la Afrika yaaniafCFTA ambalo linatoa fursa pana kwa wajasiriamali nawafanyabiashara wa KiTanzania kunufaika na soko hilikubwa, pili ajira kwa vijana ni moja ya changamoto kubwahivyo mikakati ya kukuza ujasiriamali inalenga kufanyavijana wengi kuwa na ujuzi na kujikita kwenye ujasiriamalihivyo kutumia fursa nyingi zinazotokana na ukuaji wa uchumina pia soko pana la Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Tunalenga kutengeneza kizazi cha vijana wenye kuonaujasiriamali kama njia bora ya kujiajiri na hivyo kutoka kuwawaajiriwa hadi kuwa waajiri’’.

Tanzania ina fursa nyingi sana ambazo zinahitaji jicho la kijasiriamali kuweza kuzitumia, hivyo kuwajengea uwezo waujasiriamali vijana utakuza uwezo wao wa kutambua nakutumia vizuri fursa zilizopo na zinazokuja. Kwa kutumiauwezo mkubwa wa uendelezaji biashara ilionao, EABC inalenga kutoa mafunzo na kujenga uwezo kwa vijana wengiNchini Tanzania. Kupitia ushirikiano huu na taasisi kongwena yenye mtandao mkubwa wa mikoa 26 na wilaya 150 program zetu zitawafikia na kuwanufaisha vijana wengi nahivyo kuakisi dira ya EABC ya kuwa chachu ya ukuaji waujasiriamali, alimalizia Ndugu Kajula.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Oscar Kissanga alisema ‘’ Moja kati ya malengo mahususi yakuanzishwa kwa TCCIA ni kukuza biashara nchi Tanzania, ilituweze kukuza biashara basi ukuzaji wa Ujasiriamali ninyenzo muhimu sana katika kukuza Taifa lenye wajasiamaliwanaoweza kutumia fursa zilizopo. Tunafurahi kuwaushirikiano huu unaenda kuwapa mafunzo, uzoefu na mbinuvijana ambao ni kundi muhimu kwa TCCIA. Kupitia mikakatiyetu na malengo yetu ya kuwa karibu na vijana TCCIA ilianzisha uanachama wa Vijana

Hivyo ushirikiano huu unaenda kunufaisha vijana wengiNchini Tanzania. Ni furaha yetu kama TCCIA kushirikiana nataasisi zenye malengo makubwa ya kukuza biashara naujasiriamali Nchini

Related Posts