Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank, Dkt. Ibrahim Mwangalaba Kushoto aliyekaa Mwenyekiti wa Machinga Dar es Salaam,Namoto Yusuf Namoto wakisainiMkataba wa Makubaliano ya Mradi wa kwanza wa Ununuzi wa Viwanjaa vya Wamachinga wa Kariakoo jinini Dar es Salaam leo mei 07 2024. Wa Mwisho waliyekaa ni Mmiliki wa Ardhi iliyopo kijiji cha Magoza Mkuranga, Kondo Maulid Mkangala.
Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank, Dkt. Ibrahim Mwangalaba Kushoto na Mwenyekiti wa Machinga Dar es Salaam, Namoto Yusuf Namoto wakionesha mikataba mara baada ya kusaini Mkataba wa Makubaliano ya Mradi wa kwanza wa Ununuzi wa Viwanjaa vya Wamachinga wa Kariakoo jinini Dar es Salaam leo Mei 07, 2024.
Mwenyekiti wa Machinga Dar es Salaam, Namoto Yusuf Namoto akizungumza na waandishi wa habari wakatiwa kusaini Mkataba wa Makubaliano ya Mradi wa kwanza wa Ununuzi wa Viwanjaa vya Wamachinga wa Kariakoo jinini Dar es Salaam leo Mei 07,2024. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank, Dkt. Ibrahim Mwangalaba.
KATIKA kuhakikisha Wamachinga wanakuwa na Maisha Bora, Maendeleo Bank leo Mei 07,2024 wamesaini Mkataba wa ushirikiano na Viongozi wa Kariakoo Wamachinga Association (KAWASSO) na Mmiliki wa eneo husika ili kuwajengea nyumba za makazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank, Dkt. Ibrahim Mwangalaba akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusaini Mkataba wa mara ya kwanza kwaajili ya kununua Viwanja (Machinga Plot Finance) katika eneo lililopo Mkuranga Mkoani pwani. Amesema kuwa dhamira ya Benki hiyo ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kukuza uchumi na kupunguza umasikini kwa Wananchi.
Amesema kuwa benki hiyo ilipokea maombi kutoka kwa KAWASSO ya ujenzi wa nyumba za makazi kwa wamachinga ambapo walikubaliana kuanza kununua viwanja vya Wamachinga 500 wa Dar es Salaam ili waweze kumiliki ardhi na hatimaye kupata makazi ya kuishi.
Dkt. Mwangalaba ameeleza kuwa umoja huo umeshapata hekari 89 katika kijiji cha Magonza Kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani. Kwa kutambua Changamoto inayowakabiri Wamachinga kutokuwa na dhamana zinazowawezesha kupata mikopo kupitia taasisi za fedha Maendeleo Bank imeona na kuitatua changamoto hiyo.
“Kupitia Mpango huu benki itatoa mkopo wenye thamani ya shilingi Milioni 500 kwa Wamachinga wa Kariakoo kwa awamu ya kwanza ya Mradi ili kuwezeaha kumiliki Viwanja. Hivyo pesa hizo ni kwaajili ya ununuzi wa Ardhi, Usafishaji wa eneo husika, Upimaji wa Viwanja pamoja na urasimishaji ili kuwezesha Mgawanyo wa Viwanja kwa wanachama binafsi ili kila mnufaika aweze kuwa na hati miliki ya kiwanja Chake.” Ameeleza
Dkt. Mwangalaba amesema kuwa kwa awamu ya pili kwa kushirikiana na KAWASSO na umoja wa Machinga Dar es Salaam, Maendeleo Bank itatoa mkopo wa Nyumba wenye masharti nafuu na gharama ndogo ili kuwezesha Wamachinga kumiliki nyumba ya ndogo yake.
Aidha Dkt. Mwangalaba ameeleza kuwa mpango huo utakapokamilika utawawezesha Wamachinga kumiliki ardhi na Makazi bora pia kutawaongezea sifa ya kukopesheka zaidi ili kukuza mitaji ya biashara zao na kuondoa kikwazo cha cha kutokukopesheka kwenye taasisi za fedha.
Kwa Upande wa KAWASSO, Namoto Yusuf Namoto amewashukiru Maendeleo Bank kwa imani walioionesha kwa
KAWASSO kwani taasisi nyingi za kifedha zilishindwa kuwafikia kwa sababu walikuwa hawana dhamana.