AMVUNJA MBAVU MKE WAKE KWA WIVU WA MAPENZI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi linamsaka Hamidu Abdalah kwa kosa la kumjeruhi kwa kumpiga na chaga ya kitanda mke wake Amina Athuman Said 40, mkazi wa Likongowele wilaya ya Liwale na kisha kusababisha kuvunjika kwa mbavu mbili za upande wa kulia kisha kukimbilia sehemu kusikojulikana.

Tukio hilo limehusishwa na masuala ya wivu wa kimapenzi baada ya mtuhumiwa huyo kukuta ujumbe wa maandishi kwenye simu ya mke wake huyo ambao alikuwa ametumiwa na mwanaume mwingine na ndipo ugomvi ukaanzia hapo mpaka kupelekea mtuhumiwa kuchukuwa chaga za kitanda na kumpiga nazo ambapo muhanga huyo alikimbizwa hospitali ya wilaya ya Liwale na anaendelea na matibabu.

Related Posts