PASSWORD (NYWILA) IMARA NI MUHIMU ILI KULINDA TAARIFA ZAKO KATIKA VIFAA VYA KIELEKTRONIKI NA PROGRAMU TUMIZI

Password au Nywila imara na ya kipekee ni muhimu ili kulinda taarifa zako na programu tumizi (application) zilizopo katika vifaa vyako vya kielektroniki.

Password au Nywila ni ya kwako peke yako hutakiwi kumpatia mtu mwingine, HAKIKISHA nywila hiyo ni Imara ya kipekee ikijumuisha herufi, namba na alama na ikiwezekana uwe na nywila mbili (two factor authentification) utakazotumia kufungua kifaa chako cha kielektroniki na pia kufungua programu tumizi zilizopo katika vifaa vyako.

Hii itakusaidia kulinda taarifa zako zilizopo katika vifaa vyako pindi vitakapopotea

Related Posts