Rais Mwinyi kumuwakilisha Rais Samia mkutano wa SADC

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar leo tarehe 19 Novemba 2024 kwenda Zimbabwe kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa nchi Wanachama wa SADC utakaofanyika jijini Harare.

Rais Dk, mwinyi anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, Samia Suluhu Hassan ambae ni Mwenyekiti wa Idara ya Siasa,Ulinzi na Ushirikiano wa Usalama wa SADC.

Mkutano huo wa siku mbili utajadili masuala mbalimbali ya Kikanda ikiwemo Hali ya Ulinzi na Usalama , Migogoro ya kisiasa miongoni mwa nchi Wanachama wa SADC , Tathimini ya Matokeo ya Uchaguzi na hali ya kisiasa ilivyo hivi sasa nchini Msumbiji.

 

Related Posts