ATALANTA, MAREKANI: Wote tushasikia msemo wa kwamba “Kila kwenye mwanaume mwenye mafanikio, nyuma yake kuna mwanamke.”
Msemo huo unaweza kusiikia kwenye mambo ya kisiasa na mengine, lakini je, vipi kuhusu wanawake wa mabondia, msemo huo unaleta maana?
Kama inavyofahamika, kujiandaa kwa pambano na ngumi si kazi nyepesi. Kwa kawaida inaweza kuchukua wiki hadi sita na hakuna mambo ya kujamiana, mlo wenye masharti mengi pamoja na mazoezi mazito na magumu. Unaweza kuwaza, huyo mke wa bondia, anakuwa kwenye mazingira ya aina gani? Watoto wake, wanakuwa kwenye mazingira gani?
Kuna mrembo anaitwa Livvy Cunningham, mke wa bingwa wa zamani wa masumbwi wa uzito wa Cruiser, Steve “USS” Cunningham, alifunguka kila kitu kuhusu changamoto na maisha yanavyokuwa kwa kuwa mke wa bondia.
Maswali 10 ya mke wa bondia Cunningham akifichua jinsi maisha yalivyo kwa kuelewa na mume bondia.
Swali la kwanza: Tuambie, umewezaje kuwa mke bondia?
Anajibu: Nilikutana na Steve tulikutana mwaka 2000 kwenye gym ya Biggs Morrison Boxing Gym, Atlanta. Nilihamia huko baada ya kuhitimu kwenye Chuo Kikuu cha Boston na Steve naye alihamia hapo baada ya kuondoka kwenye jeshi la Marekani. Nilikuwa najifunza masumbwi ili kuweka mwili sawa naye alikuwa akifanya mazoezi hapo kama bondia wa ngumi za ridhaa. Aliniomba tutoke kwenda muvi na hivyo ndivyo ilivyokuwa, ambapo tangu kipindi hicho tumekuwa pamoja.
Umekuwa na Steve katika maisha yote ya masumbwi?
Anajibu: Ndiyo, tumekuwa pamoja kwa kipindi chote cha kujihusisha na mchezo wa masumbwi. Tulikutana kipindi akiwa bado anapigana ngumi za ridhaa hadi alipopanda na kuhamia kwenye ngumi za kulipwa. Aliingia kwenye ngumi za kulipwa muda fupi baada ya mimi na yeye kuanzisha uhusiano.
Swali la tatu: Imekuwaje safari yako ya kuwa mke wa bondia?
Anajibu: Imekuwa ya aina yake. Tumebarikiwa sana. Imekuwa safari ya misukosuko na wasiwasi mwingin, lakini sina ambacho naweza kukibadilisha. Sote tumekuwa na malengo yanayolingana na kufanya kazi kama timu. Nilitaka awe bingwa wa dunia na niliamini hivyo siku zote. Kwa miaka mingi, mimi niliweka bidii kwenye kufanya kazi kwa ajili ya kusapoti familia ili yeye apate muda wa kutuliza akili kwenye mazoezi, awe bora na bondia mahiri ulingoni. Na hilo lilifanikiwa. Ni bingwa wa dunia zaidi ya mara moja. Sasa tufanyakazi pamoja, mimi ni meneja wake na tumekuwa na biashara nyingine tulizowekeza nje ya mchezo wa masumbwi.
Swali la nne: Ni nyakati gani ngumu za kuwa mke wa bondia wa kulipwa?
Anajibu: Kwangu mimi, ni nyakati ninazomwona mume wangu akipigwa kwenye pambano. Si kwa sababu ya sifa, rekodi au pesa, bali ni kwa sababu anavyofanya jitihada za kupambana ili kuwa bondia mzuri. Nataka apate sifa kubwa duniani, kwa sababu anastahili. Sipendi kuona amehuzunika, inanivunja sana moyo. Lakini, mwisho wa yote hayo, tunafahamu kwamba Mungu ana mpango na sisi, kushinda, kupoteza au kutoka sare basi maisha lazima yaende. Lakini, zinakuwa siku ngumu baada ya kupoteza pambano.
Swali la tano: Ukiwa kama mama, unaona wanao wakiingia kwenye hizi biashara za familia?
Anajibu: Ukweli nina changanyikiwa kwenye hilo. Sina mawazo ya aina moja. Vijana wetu siku zote wanakwenda gym, wanakuwa na wanakwenda kufanya mazoezi gym. Ni lazima, lakini sio kwenye kupigana. Tunataka wawe na ujuzi na nidhamu tu, lakini hatutaki wapigane, hicho ndicho tunachokitaka. Lakini, kama wenyewe wataamua kujifunza ngumi kwa ajili ya kuwa mabondia halisi, basi tutawasapoti asilimia 100.
Swali la sita: Unaweza kutueleza usiku wa pambano la mumeo unavyokuwa kwako?
Anajibu: Unapofika usiku ambao mume wangu ana pambano, nakuwa najisemesha mwenyewe, ‘kwanini tunafanya hii kitu?’. Huwa naona kama tumbo linaunguruma hivi. Kwa upande wangu ni ngumu sana, nakuwa nafanya maombi mengi sana kumtegemea Mungu. Kwa siku nzima, nakuwa sina raha, Steve yeye anakuwa amepumzika, tunakuwa na chakula cha watu wote ukiwa ukumbini. Nikifika ukumbini, nasubiri vyumbani hadi tutakapokwenda pamoja ulingoni, kisha naketi kwenye kiti changu macho yote ulingoni.
Kengele ya pambano inapogongwa, pambano likianza, huo ndio wakati mgumu zaidi kwangu, natazama pambano kama vile nipo kwenye njozi. Ninachokuwa nawaza ni kusikia tu kengele ya mwisho wa pambano. Ukweli hakuna kitu kizuri kama akiwa ameshinda pambano! Baada ya hapo narudi vyumbani na kuzungumza na waandishi wa habari kwa furaha kubwa. Lakini, pambano linapomalizika wote tunakuwa na njaa ya hatari na kutafuta chakula.
Swali la saba: Kitu gani kinakua akili mwako Steve atapokuwa ulingoni?
Anajibu: Nataka pambano liishe, iwe kwa ushindi, sare au kupoteza, yani liishe tu. Kitu ambacho nimekuwa nikifanya ni kuomba dua ashinde, lakini muda wote nimekuwa makini kwenye kuhesabu raundi na kuomba Mungu muda wote. Nakuwa napiga kelele sana kwa sababu nataka ajue kona yake ni ile na nimekuwa nikiwaambia wanaosimamia mambo kibao. Lakini, zaidi nakuwa najivunia sana nikimwona ulingoni, kwa sababu ni mpambano mahiri na napenda anachofanya.
Swali la Nane: Kuna chochote ungependa watu wajue ugumu wa kuwa mke wa bondia?
Anajibu: Kuna mengi sana zaidi ni kujitoa mhanga. Tangu nilipoanza kufanya kazi kama meneja wa Steve, nimekuwa nikijihusisha kwenye mambo mengi ya masumbwi na hilo ni jambo gumu sana. Kumekuwa na presha kubwa sana katika kuhakikisha wanaume wetu wafanya vizuri na kuweza kupigana kwa ubora katika kila pambano, hivyo anapambana sana. Ni ngumu pia kuona kwamba mumeo lazima apigane ili kupata kitu cha kulisha familia.
Swali la tisa: Pambano gani la mumeo lilikuwa gumu kulitazama?
Anajibu: Hiyo ni ngumu kusema, lakini nadhani ni lile pambano la Adamek. Lile ni pambano la kwanza ambalo aliangushwa mara tatu na lilikuwa la kwanza kupoteza. Lilikuwa ni pambano liliangaliwa sana, lakini ukweli kwangu mimi lilikuwa pambano gumu kulitazama. Nilikuwa nahesabu raundi zote za mume wangu alizoangushwa. Ilikuwa ngumu sana.
Swali la kumi: Je, unakwenda ulingoni kwenye kila pambano?
Anajibu: Ndio, nakwenda kwenye mapambano yote ya Steve. Hata lile pambano dhidi ya Kelvin Davis, ambalo nilikuwa na ujauzito wa miezi minane na nusu wa binti yetu, Kennedy. Nilisafiri kwenye Afrika Kusini kutazama pambano hilo, nilitumia muda mwingi sana angali kuliko ardhini, lakini niliamini kuwapo ulingoni kungempa nguvu zaidi mume wangu na hilo lilikuwa muhimu kwetu zote.