Ras Morogoro atoa agizo kwa EWURA ,vituo vya mafuta vyadaiwa kuwaibia wateja mafuta

Katibu tawala Mkoa Morogoro Alhaj Dokta Mussa Ally Mussa ameitaka Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) kufuatilia vipimo vya mafuta katika vituo vya kujazima mafuta kwani kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu uchakachuaji wa vipimo.

Dokta Mussa ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa Wadau EWURA kanda ya Kati ulifanyika mjini Morogoro ambapo anasema ofisi yake imepokea malalamiko mengi kuhusu baadhi ya vituo vya mafuta kufanya udanganyifu kwa wateja wao.

Anasema mafuta yanayojazwa ni tofauti ni fedha halali jambo ambalo kimekua usumbufu mkubwa Kwa wateja na kuanzia kulaalamika, hivyo EWURA wanatakiwa kufuatilia Ili kujua ukweli wa jambo hilo .

Aidha Dokta Mussa amezumgunzia changamoto nyingine ya ujazo katika gesi za mjumbani ambapo inauzwa bila kupimwa uzito na wateja wameonekana Kukosa elimu ya utambuzi wa ujazo sahihi.

Kwa upande wake Hawa Hassan Lweno Meneja EWURA kanda ya Kati amesema lengo la Mkutano huo kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuwasilisha malalamiko pindi wanapokutana na changamoto kwenye sekta ya maji,Mafuta ,gesi na umeme .

Aidha ametoa Wito kwa makampuni yenye vituo vya jujazia mafuta na gesi kuhakikisha wanatoa vipimo sahihi Kwa wateja Ili kuepukana na adhabu mbalimbali wanazoweza kukumbannazo pindi watakapobainika kufanya udanganyifu .

Juma Mpinde mmoja wa madereva bajaji anasema mara kadhaa amekumbana na changamoto ya kushindwa kupata mafuta stahiki wakati wa ujazo wa mafuta Kwenye vituo vya kujazima mafuta.

Anasema licha ya kukumbana na changamoto hiyo aidha analazimka kutengeneza bajaji yake mara kwa mara kutokana na mafuta anayokumbana nayo kukosa ubora na kuharibifu vifaa vya chombo hicho.

Naye Amina Ally mmoja wa wafanyabiashara wa mafuta katika kituo cha kujazima mafuta anasema suala la ubora wa mafuta sio kosa lao kwani ya aletwa tayari yakiwa yamechakachuliwa hivyo serikali inatakiwa idhibiti changamoto hiyo kuanzia bandarini .

 

Related Posts