Happi ahimiza kampeni zenye staha ili kuwapata viongozi bora

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Ally Hapi amewataka viongozi wa chama cha mapinduzi na vyama vingine kufanya kampeni za kistaaribu na kiungwana ili kuendelea kulinda amani na mshikamano uliopo nchini huku akihamasisha wagombea kujikita katika kueleza sera zao badala ya kutumia majukwaa kueneza siasa za chuki

 

Hapi, amehutubia mamia ya wananchi na wanaccm wa Bukoba akihamasisha umuhimu wa kuchagua viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

 

Katika hotuba yake, Hapi alisisitiza kuwa viongozi wa CCM wamekuwa na rekodi bora ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya elimu, afya, na maji chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Related Posts