KATIBU MKUU WA NLD AZINDUA RASMI KAMPENI HANDENI, ATOA WITO KWA VIONGOZI VYAMA VA SIASA KUFANYA SIASA ZA KISTAARABU


Na Oscar Assenga,HANDENI.

KATIBU Mkuu wa Chama cha NLD Doyo Hassan Doyo amezindua rasmi kampeni za wagombea wa chama hicho kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kata ya Kwedukwazu wilayani Handeni huku akitoa wito kwa viongozi wa chama hicho hapa nchini wafanye siasa za kistaarabu ambazo haziendi kutweza utu wa mtu.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu ambapo vyama vya siasa ambazo zimeweka wagombea zitachuana ili kuweza kuwapata washindi ambao wataongoza Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji na wajumbe wa mitaa katika maeneo mbalimbali nchini.

Doyo aliyasema hayo mara baada ya kuzindua rasmi kampeni za chama hicho katika Kijiji cha Kwedikwazu Magharibu Kata ya Kabuku wilayani Handeni mkoani Tanga ambapo katika pamoja na mambo mengine aliwanadi wagombea ambao watachuana na vyama vyengine kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Alisema anatoa wito huo kwa sababu chama cha siasa kina kazi kubwa ya kuwaunganisha watanzania na chama ambacho kitawa sambaratisha wasikipe nafasi katika uchaguzi huo ambao ni muhimu kwa maendeleo.

“Nitoe wito kwa Chama changu cha NLD sehemu tunazokwenda kufanya kampeni tufanye siasa za Kistaarabu ambazo zinakwenda kuwaunganisha watanzania na sio vyengivyo”Alisisitiza Katibu Mkuu huyo wa chama cha NLD.

Aidha pia alitoa wito kwa vyama vyote za siasa ambazo vimesimamisha wagombea katika uchaguzi huo wasifanye kampeni za kukwaza watu bali viheshimu watu na vinadi sera ili watanzania waweze kuamua chama gani kinaweza kuwasaidia katika kipindi cha miaka mitano ngazi ya mtaa na vitongoji.

“Huu ni wito nautoa kwa viongozi wa chama cha NLD nchi mzima wahakikisha wanafanya kampeni za kistaarabu na wasifanye zile ambazo zinakwenda kukwaza watu bali waheshimu watu na tunadi sera ili uchaguzi ukiisha waendelee kuheshimiana”Alisema

Alisema wameamua kuzindua kampeni hizo katika Kijiji hicho kutokana na kwamba kwenye vitongoji 10 NLD imepata wagombea vitongoji vyote wakiwemo wajumbe, Mwenyekiti na wale wa viti maalumu ambao watachukua na vyama vya upinzani katika kinyang’anyiro hicho.

Awali Mwenyekiti wa NLD wilaya ya Handeni Rajabu Zakaria Doyo alimuomba Rais Dkt Samia Suluhu watupie macho kwenye ngazi ya usimamizi wa uchaguzi kwenye wilaya kwa sababu kuna katatizo ambako wenzao wanakileta wakati wa uchaguzi.

Alisema kwa sababu wanapokwenda kusimamia watu kwa bunduki kwani watu hawagombani na wasimamizi ni mawakala ambao wamewateua na wao wanawasainisha na kisheria.

“Chumba cha kura hairuhusiwi mtu kuja na bunduki katika chumba cha kura wala kueleza kwamba wao ni viongozi wakubwa kwa sababu kuna watu wameteuliwa kusimamia uchaguzi huo lakini kubwa tumejipanga kufanya kampeni za kistaarabu”Alisema Mwenyekiti Rajabu.



Related Posts