Ruto afutilia mbali mkataba tata na kampuni ya Adani – DW – 21.11.2024

Muda mfupi baada ya saa nane, Rais William Ruto alipokelewa na naibu wake mpya Profesa Kithure Kindiki aliyeapishwa wiki tatu zilizopita.

Kama ilivyo ada, alikagua gwaride la heshima aliloandaliwa kabla ya kuingia bungeni kulikofanyika kikao cha pamoja cha wabunge na maseneta. Hii ilikuwa hotuba ya pili ya hali ya taifa, tangu Ruto alipoingia madarakani.

Soma: Marekani yamshtaki bilionea wa kampuni ya India ya Adani kwa hongo

Katika tukio ambalo halikutarajiwa, Rais William Ruto ametangaza kufutilia mbali mikataba na kandarasi za kampuni ya Adani iliyotarajia kumiliki uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA na usambazaji wa huduma za umeme kupitia kampuni ya KETRACO.Rais William Ruto alisema,’’Nimewaamuru wahusika kwenye wizara ya uchukuzi na nishati na petroli kufutilia mbali haraka iwezekanavyo mkataba wa kupanua uwanja wa JKIA kwa ushirikiano na Adani…. Pamoja na ule wa Ketraco wa umeme na kusaka washirika wapya kwani hii ni miradi muhimu.

Gautam Adani
Mwenyekiti wa kampuni ya Adani Gautam AdaniPicha: Sam Panthaky/AFP/Getty Images

Chini ya mkataba huo, kampuni ya Adani inayoandamwa na kashfa, ingepata nafasi ya kufanya ukarabati na kumiliki uwanja wa kimataifa wa JKIA kwa muda wa miongo mitatu jambo lililozua hisia mseto.Mtazamo wa wakenya ni kwamba wanataka kuona hela mikononi mwao ili maisha yaweze kuendelea kwani hali ni ngumu wanaelezea baadhi.Kulingana na mbunge wa Molo ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya fedha anaamini kuwa,’’Rais ameonekana kuwa kiongozi anayesikiliza kilio cha wakenya. Kadhalika mkataba wa Adani ulikuwa haujamaliziwa kufanyiwa kazi kwahiyo ni sawa ukifutiliwa mbali na tujipange upya.”anafafanua.

Uchumi waimarika na kukua kwa 5.6%

Kwenye hotuba yake ya taifa , Rais William Ruto alisisitiza kuwa mambo yameimarika hususan uchumi ambapo mfumko wa bei umepungua kutokea 9.6% mwaka 2022 hadi 2.7% katika mwezi wa Oktoba mwaka huu.Kiwango hicho ni cha chini kabisa kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 17.Amenya asema maisha yako hatarini

Kuhusu bima mpya ya afya ya SHIF na mamlaka ya afya ya SHA, kiongozi wa taifa alifafanua kuwa malipo yote yatafanyika kikamilifu kuanzia wiki ijayo.Dhamira ni kuhakikisha kuwa utoaji wa huduma za afya ya msingi unaimarika kila uchao.Charles Kamuren ni mbunge wa Baringo kusini na anahisi kuwa,” Rais ametoa hotuba inayoendana na wakati kwani anawasikiliza wakenya.Ameangazia mpangilio uliopo wa kuimarisha elimu na pia ajira kwa vijana.Hayo ni mambo mazuri ,” anamalizia.

Kenya | Nairobi | JKIA
Uwanja wa ndege wa Kenya Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

William Ruto amelihakikishia taifa kuwa nchi iko kwenye mkondo sawa ukizingatia masuala ya chakula cha kutosha kwani ghala la taifa linahifadhi magunia milioni 47 ya mahindi,milioni 8.8 ya maharagwe, ngano na mchele.Kadhalika ameelezea kuwa tangu Februari,serikali imegawa mbolea iliyopunguwa bei kwa wakulima milioni 6.5 waliosajiliwa kwenye kaunti 47 jambo lililoliongeza mavuno.Wafanyakazi wa JKIA wasitisha mgomo huku wakiionya serikali dhidi ya kuruhusu kampuni ya India ya Adani kuchukua mamlaka ya usimamizi wa uwanja huo

Kimsingi, kiongozi wa taifa amebainisha kuwa hatua zimepigwa ijapokuwa changamoto zipo.Hii ni hotuba ya kwanza ra rais Ruto tangu kupata naibu mpya ambaye ni Profesa Kithure Kindiki aliyechukua nafasi ya Rigathi Gachagua aliyetimuliwa kwa makosa ya uongozi mbaya na ufisadi. Bunge la taifa na baraza la senate limeahirisha vikao hadi wiki ya mwisho ya Novemba.

Related Posts