ICC Yatoa Hati ya Kukamatwa kwa Netanyahu, Gallant na Al-Masri kwa Uhalifu wa Kivita Gaza

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu imetoa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, aliyekuwa waziri wa ulinzi Yoav Gallant pamoja na kiongozi wa Hamas Ibrahim Al-Masri kwa tuhuma za uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu katika mzozo wa Gaza uliosababisha vita kuanzia Oktoba 8, 2023 mpaka Mei 20, 2024.

Kwa mujibu wa Reuters uamuzi wa majaji wa ICC umeeleza kuna sababu za kuridhisha za kuamini kuwa Netanyahu na Yoav Gallant walihusika na vitendo vya uhalifu ikiwa ni pamoja na mauaji, mateso na njaa kama silaha ya vita na sehemu ya mashambulizi makubwa na ya kimfumo dhidi ya raia wa Gaza.

Related Posts