STELLA IKUPA AFANYA ZIARA VITUO VYA WASAFIRISHAJI BAJAJI ZA WATU WENYE ULEMAVU MKOA WA DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Viti Maalum, anayewakilisha watu wenye ulemavu Tanzania, Mh.Stella Ikupa, amefanya ziara katika vituo vya watu wenye ulemavu, wasafirishaji abiria kupitia bajaji ndogo na kubwa, katika Jiji la Dar es Salaam.

Vituo alivyotembelea Mbunge Mh. Stella ni Nyahaja Uhasibu Group kilichopo pembezoni mwa Chuo Cha Uhasibu (TIA), Temeke, Kituo cha Ocean Road cha bajaji ndogo cha wanawake, kituo cha bajaji kubwa na ndogo cha feli cha wanaume,(UWABADA) kituo cha wanaume cha Mnazi Mmoja (UWABAKUTA).

Akizungumza katika vituo hivyo, Mbunge Mh.Stella Ikupa, amewapongeza wasafirishaji hao wenye ulemavu kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia kuisemea vizuri kwa kazi kubwa zinazotelezwa na serikali.

Mbunge Mh.Stella, amewasisitiza wasafirishaji hao, kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Mh. Rais Dkt.Samia kwa kujitokeza kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Lengo la kuwafikia siku ya leo ni kuwahamasisha na kuwakumbusha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulioko mbele yetu, unaotarajiwa kufanyika Jumatano Novemba 27, kwani ni haki ya kila mwananchi kumchagua kiongozi anayemtaka.

“Lakini zaidi muwachague wagombea wa CCM, kwasababu ya kazi kubwa inayofanywa na Mh. Rais Dkt.Samia nchini ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya barabara, afya, maji kuondoa kero mbalimbali za wananchi,” alisema.

Alisema, serikali ya Rais Dkt. Samia haijawasahau watu wenye ulemavu, kwani imeendelea kutoa mikopo ya asilimia kumi isiyo na riba ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa walemavu na kuwasaidia kukuza uchumi wao.

Mbunge Mh.Stelaa alisema serikali ya Rais Dk.samia imeweka mazingira wezeshi kwa walemavu kufanya shughuli zao, ikiwemo kuruhusiwa kufanya shughuli zao katikati ya majiji hususan Jiji la Dar es Salaam jambo ambalo limeendelea kuleta tija kubwa kwao.

“Hakika, tunayosababu kubwa ya kuichagua CCM katika Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, kwani imetugusa walemavu kwa sehemu kubwa, bila kusahahu kujenga miundombinu wezeshi kwa walemavu katika miradi mbalimbali ikiwemo ya afya na maji na usafirishaji,” alisema.

Katika hatua nyingine, Mh.Mbunge Stella, alisikiliza changamoto mbalimbali za walemavu huku zingine akizitolea ufafanuzi ikiwemo Ile ya mikopo ya asilimia 10 isiyo na riba.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makada wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Pili Birahi alimpongeza Mbunge Stella kwa ziara hiyo muhimu ya kuwafikia watu wenye ulemavu jambo ambalo limekuwa faraja kubwa kwao.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Nyahaja Uhasibu Group, Makamba Amiri alimshukuru Mbunge Mh. Stella, huku akiahidi kumuunga mkono kwa kuhakikisha anawahamasisha wajumbe na watu wengine wenye ulemavu kupiga kura.

Naye, Diwani wa Kata ya Kivukoni, Shariki Choughule alisema wamefurahishwa na ziara ya Mbunge Mh.Stella, katika kata yake kukutana na watu wenye ulemavu , huku akiwasisitiza kuwachagua viongozi wa CCM, ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais Dk.samia kwa kutoa fedha nyingi za maendeleo .

Vilevile, Mwenyekiti wa Madereva wa babaji za watu wenye ulemavu Tanzania (WABAKUTA), Mathew Kasiririka alisema wako tayari kuiunga mkono serikali ya Rais Samia kuwachagua viongozi wa CCM katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwani imewapa uhuru wa kufanya shughuli zao kwa amani.


Related Posts