Wafamasia wataka utafiti kupata dawa za nguvu za kiume Tanzania

Chama Cha Wafamasia Tanzania PST, Kanda Ya Nyanda Za Juu Kusini Kimetoa Wito Kwa Serikali Ya Tanzania Kuweka Mkazo Katika Utafiti Wa Ndani Ili Tanzania Iweze Kuwa Mzalishaji Wa Dawa Za Binadamu Ikiwemo Zinazotibu Tatizo la Nguvu za Kiume

Mwenyekiti Wa PST Kanda Ya Nyanda Za Juu Kusini Jackson Nzinza Ametoa Kauli Hiyo Leo Katika Ziara Ya Viongozi Wa Chama Hicho Kwenye Bohari Ya Dawa Na Hospitali Ya Rufaa Mkoa Wa Iringa Kuhimiza Mafamasia Kujiunga na PST

Amesema Kuwa Kutokana Na Uwepo Wa Dawa Mbalimbali Zinazodaiwa Kutibu Tatizo La Nguvu Za Kiume Hapa Nchini Serikali Inaweza Kuweka Kipaumbele Katika Utafiti Wa Dawa Hizo Ili Kupata Tiba Iliyothibitishwa

Ziara hiyo pia ililenga kuhamasisha wanataaluma kushiriki Mkutano Mkuu wa Wafamasia unaotarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 4 hadi 6, mwaka huu, jijini Dodoma.

Nzinza ameelezea umuhimu wa kufanya utafiti wa kina kuhusu dawa ya mkuyati, inayotumika sana miongoni mwa jamii ya Wamaasai.

Naye Robert Lugembe ni Mfamasia na Meneja wa Bohari Kanda ya Iringa, amesema viongozi wa wafamasia wamepata fursa ya kujifunza jinsi wanavyohudumia wateja na kuwahamasisha wanachama kuwa na umoja katika utekelezaji wa kazi zao.

Kwa upande wao, Jojina Fredric Kabugumila, Mfamasia kutoka Hospitali ya Rufaa ya Iringa, na Dr. Veronica Mahembe kutoka Hospitali ya Rufaa Mbeya, wameishukuru serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha upatikanaji wa dawa kwa wakati, tofauti na kipindi cha nyuma.

Related Posts