DJ na Mwanamuziki anayekuja kwa kasi Deejay Val kutoka nchini Nigeria, amedondosha wimbo mpya uitwao LEKKI BADDIE, unaopatikana kwenye EP yake mpya iitwayo FUSION yenye jumla ya ngoma tano.
Deejay Val amefanyia remix wimbo huo na wasanii mbalimbali wa Afrika na anaelekea kuteka soko barani Afrika na Ulaya
Valentine Ejimbe, maarufu kama Deejay Val, anatoka Nnewi, jimbo la Anambra. Aliingia kwenye sekta ya burudani mnamo 2014 kama DJ. Baadaye aliingia kwenye muziki mwaka 2019, na wimbo wake wa kwanza akiwa na wasanii kadhaa kutoka Mashariki.
Aliachia kazi yake ya kwanza, GOD IS A DEEJAY, mwaka 2020. Tangu wakati huo, ameendelea kuachia kazi nyingi bora zenye kuleta mshangao.