Slads kuwahusisha Alumni katika maendeleo ya chuo

Mkuu wa chuo cha ukutubi na uhifadhi nyaraka (slads),Bertha Mwaihojo siku ya jana alipata wasaa wakuwasihi wanafunzi wa sasa na wale waliohitimu miaka ya nyuma katika chuo hicho kilichopo Bagamoyo mkoani pwani kwenye kongamano la umoja wa wanafunzi waliowahi kusoma Slads na kuwahusisha wote katika maendeleo ya chuo hicho.

Mkuu huyo wa chuo Bi,Bertha Mwaihojo aliyasema hayo kwenye hotuba yake fupi mbele ya mgeni rasmi Dr.Mboni Ruzegea na kumweleza kuwa kongamano hilo lina malengo makuu matats nayo ni kuimarisha mshikamano na mtandao wa alumni,kushirikishana Maarifa na uzoefu na mwisho kuwahusisha alumnai katika maendeleo ya chuo.

Aliongeza kusema pia licha ya malengo walionayo lakini pia chuo hicho cha Slads kina changamoto zake nazo ni miundombinu ya Tehama kufwatiwa na ongezeko la wanafunzi na mabadiliko ya Tehama katika kufunza na kujifunziq,pia maktaba ya chuo hicho ni ndogo hali hai inapelekea kiwa na huduma duni.

Bi.Bertha Mwaihojo alimaliza kwa kuwashukuru wote na kuwahimiza wanafunzi kujihusisha na ushirika,vile vile kutafuta ushauri kujenga muungano kati ya wao kwa wao.

Related Posts