CCM HATUCHEKI NA MTU KATIKA KUSHIKA DOLA,TUMEJIPANGA- CPA MAKALLA

Na Mwandishi Wetu

KATIBU wa Halmashauri Kuu ( NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Itikadi, Uenezi, Siasa na Mafunzo CPA Amoss Makalla amesema Chama hicho hakicheki na mtu katika kushika dola na katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu wamejipanga kuhakikisha wanashinda kwa kishindo.

CPA Makalla ameyasema hayo leo Movemba 23,2024 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka.

Amesema kuwa kwa sasa Chama hicho limeendelea kufanya kampeni za Uchaguzi huo na walizindua kampeni zao rasmi Novemba 20 mwaka huu katika mikoa yote nchini na tangu kuanza kampeni hizo wagombea wa Chama hicho wataibuka na ushindi wa kishindo .

“Katika uchaguzi huu wa Serikali ya Mitaa tutashinda na tunataka ushindi wa kishindo.Kwa jinsi ambavyo CCM tumejipanga ni sawa na kusema yanayoendelea ni sawa na kusema yajayo yanafurahisha,”amesema CPA Makalla.

Akisisitiza zaidi amesema uchaguzi huo ni muhimu na CCM inachukulia uchaguzi huo kwa umuhimu mkubwa kwani inatambua kazi ya chama cha siasa ni kushika dola na Chama hicho kinaanza na kushinda uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Kazi ya Chama cha siasa kilichosajiliwa ni kuhakikisha kinashika dola maana kazi ya kuhubiri kwenda mbinguni hiyo inafanywa na viongozi wa dini.Kwa kutambua umuhimu wa kushika dola ndio maana katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa CCM imeweka wagombea wake kwa asilimia 100 kwani hakuna Mtaa,Kijiji Wala Kitongoji ambacho tumeacha,kote tumesimamisha wagombea a kwa nafasi zote.

“Vyama vingine havina utayari na ndio maana wameshindwa kusimamisha wagombea katika nafasi zote na mpaka sasa kuna Mitaa ambayo tayari wagombea wake hawana washindani,”amesma CPA Makalla na kuongeza katika maeneo ambayo wapinzani hawajasimamisha wagombea kampeni ziendelee maana kutakuwa na ndio au hapana.

Hata hivyo amesema katika maeneo ambayo wapinzani hawajasimamisha wagombea wamepanga kupiga kura ya hapana lakini akiwaangalia haoni kama wanaoubavu huo kwani kama wameshindwa kuweka wagombea ubavu wa kuzuia wagombea wa CCM wasishinde wanautoa wapi.

“Kwa wapinzani wanaofikiri wanaweza kuiangusha CCM kwa kura za hapana ni sawa na kusubiri meli katika uwanja wa ndege ni jambo ambalo haliwezekani.”

CPA Makalla amesema kampeni za uchaguzi huo zimebakisha siku tatu lakini amesisitiza kwamba kama ambavyo wamezindua kampeni kwa kishindo na watafunga kampeni kwa kishindo na katika hilo wamejipanga vizuri.

“Tangu tulipozindua kampeni, zinaendelea vizuri na maelfu ya wapinzani wanarudi CCM na kuna wagombea wa vyama vingine na wenyewe wanataka kujiunga na CCM.Kampeni zetu tutazifunga kama tulivyofunga.”

 

Related Posts