DKT. SAMIA ATUNUKIWA SHAHADA YA UDAKTARI WA HESHIMA YA UONGOZI

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Udaktari ya Heshima (PhD) katika uongozi, leo tarehe 24 Novemba 2024, kwenye mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, yaliyifanyika Kampasi Kuu ya Morogoro.

Shahada hiyo aliyotunukiwa Mhe. Rais Dkt. Samia, imetokana na umahiri na uwezo aliouonesha kwenye uongozi katika nafasi mbalimbali alizotumikia taifa, kupitia Chama na Serikali na nje ya hapo. Pia Dkt. Samia leo ni mgeni maalum kwenye mahafali hayo yanayofanyika katika Viwanja vya Maekani.

Related Posts