KAMPUNI inayoongoza katika Teknolojia na Mawasiliano,Vodacom Tanzania Plc kwa kushirikiana na Sanlam Investments East Africa Limited, leowamezindua M-Wekeza, huduma ya kibunifu ya uwekezaji iliyoundwa ili kuleta fursa rahisi za uwekezaji kwa watumiaji wa M-Pesa kupitia njia ya kidijitali ya simu zao za mkononi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
M-Wekeza inawawezesha watumiaji kuanza kuwekeza kwa kiasi kidogo cha shilingi 10,000/=, ikitoa faida ya ushindani ya hadi asilimia 13 ya riba kwa mwaka. Huduma hii ya kisasainaashiria kuingia kwa Vodacom M-Pesa katika masoko ya mitaji, ikileta fursa mpya za ukuajiwa kifedha kwa Watanzania na kuendeleza dhamira ya kampuni hiyo ambayo ni kukuzaushirikishwaji wa kifedha.
Huduma hii inayoletwa kwa kushirikiana na Sanlam Investments East Africa Ltd, mshirika wauwekezaji aliye na leseni na sifa nzuri, inalenga kurahisisha mchakato wa uwekezaji kwa kilaMtanzania, na kuwawezesha kuongeza kipato chao kwa kuwekeza kwenye vyombo kamadhamana za serikali, masoko ya hisa na masoko mengine ya mitaji salama. Huduma hiiinaendana na malengo ya Vodacom ya kukuza ushirikishwaji wa kifedha na kutoa hudumambalimbali za kifedha kupitia M-Pesa.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi wa M-Pesa Epimack Mbeteni alielezeafuraha yake kwa kuzinduliwa kwa huduma hii, akisema, “M-Wekeza ni hatua nyingine muhimukatika dhamira yetu ya kuwawezesha Watanzania, kwa kutoa huduma mbalimbali za kifedhakidigitali. Tumebuni huduma hii ili iwe rahisi, ipatikane kwa wote na yenye kuwaletea faida. Iwewewe ni mwekezaji mzoefu au mpya, M-Wekeza inatoa fursa salama na rahisi ya kuongezakipato chako kupitia simu yako ya mkononi.”
M-Wekeza inadhibitiwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Usalama (CMSA), ambayoinahakikisha uwazi na usalama hivyo kuleta imani kubwa katika mchakato wa uwekezaji. Kwa usimamizi imara kutoka CMSA, M-Wekeza inatoa njia salama na ya kuaminika kwa watumiajiwa M-Pesa kushiriki katika masoko ya mitaji yanayokua ya Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa CMSA, Nicodemus Mkama, alisisitiza umuhimu wa huduma hii: “Uzinduzi wa M-Wekeza ni hatua ya mabadiliko kuelekea kurahisisha upatikanaji wa fursa za uwekezaji hapa Tanzania. Ushirikiano huu kati ya Vodacom, Sanlam Investments na CMSA unaleta daraja linalowaunganisha Watanzania na masoko ya mitaji na hivyo kuwawezesha watukutoka tabaka zote za kijamii kuwekeza na kujenga mustakabali wao wa kifedha.”
Jonathan Stichbury, Mkurugenzi Mtendaji wa Sanlam Investments East Africa, pia alizungumziaushirikiano huu akisema, “Sanlam Investments, tumejidhatiti kukuza ushirikishwaji wa kifedhakupitia suluhisho za kibunifu. Ushirikiano wetu na Vodacom ni hatua muhimu katika kuleta fursaza uwekezaji zinazoweza kufikiwa na zinazovutia kwa Watanzania. M-Wekeza sio tu inatoa ribaya kila siku kwa mapato, bali pia inaruhusu kutoa pesa papo hapo, hivyo kufanya uwekezajikuwa rahisi na haraka kwa kila mtu.”
Uzinduzi wa M-Wekeza unaimarisha zaidi uongozi wa Vodacom M-Pesa katika sekta ya hudumaza kifedha za kidijitali na kuimarisha dhamira ya kampuni ya kuwawezesha Watanzania kwafursa kubwa za ukuaji wa kifedha, ushirikishwaji na usalama wa fedha zao.