Mwigulu amkabidhi mkandarasi mradi wa umwagiliaji wenye thamani ya Bilioni 10 Iramba

Waziri wa Fedha na Mbunge wa Iramba Magharibi, Dkt Mwigulu Nchemba ,Novemba 22 .2024 amemkabidhi Mkandarasi Otonde Construction, ujenzi wa mradi wa skimu ya umwagiliaji wenye thamani ya Billion 10 utakaohudumu katika kata ya urughu ,kijiji cha Masimba wilayani Iramba.

Akizungumza katika hafla hiyo Mwigulu amesema kuwepo kwa mradi huo kutakuwa na tija kubwa kwa wakazi wa iramba hasa kata ya urughu kwani moja kwa moja watu wataondokana na umasikini ,hata hivyo Nchemba ameongezea kwa kusema kuwa si jambo lililozoeleka kwa vijiji kupatiwa miradi yenye fedha nyingi lakini serikali ya Samia imekuwa kawaida kwake kutoa fedha nyingi kwa ajili ya wananchi kama ilivyofanyika masimba

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda ameshukuru kuwepo kwa mradi huo katika wilaya yake huku akisema wilaya ya iramba iko salama hususani katika eneo la chakula.

Wananchi wa kijiji cha masimba wamepongeza serikali kuwapelekea mradi huo kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji japo wametuma salamu katika wizara ya kilimo kwa kuwataka kuhakikisha mradi huo unamalizika mapema na kwa aslimia mia moja kama ambavyo imezungumzwa.

Mradi huo uliokabidhiwa leo kwa mkandarasi unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 12 yaani utakamilika December 5 .2025 ,na zaidi ya wakulima 500 watanufaika na skimu hiyo huku zaidi ya hekari 1000 zinaenda kutengenezwa.

 

Related Posts