MAAMBUKIZI YA UKIMWI YAONGEZEKA NCHINI KWA VIJANA RIKA BALEHE KATI YA MIAKA 15_24

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali TACOSODE  Koga Mihana ikiwa katika wiki ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani amesema takwimu zinaonyesha waathirika wakubwa wa maambukizo ya virusi vya UKIMWI duniani ni vijana wenye kundi kuanzia umri wa miaka 15-24 ambayo ni takwimu ya mwaka 2024 ukiwa ni moja kati ya umri ambao unakumbana na changamoto ya maisha ya ujana na teknolojia 

Akiainisha sababu kadhaa ambazo hupelekea vijana kua na maambukizi ya virusi vya UKIMWI ambapo idadi kubwa ni watoto wa kike hali inayotokana na dunia kukua katika kipindi cha kasi ya kukua kwa teknolojia, tabia hatarishi na tamaa ya maisha mazuri.

Aliongeza kwa kusema kupitia wiki ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani  taasisi ya TACOSODE wamejipanga katika utoaji wa elimu ambapo utalenga makundi tofauti tofauti wakiwemo walimu wa shule za msingi na sekondari,wazazi na vijana ambao watapewa elimu kuhusiana na njia za kujikinga na virusi vya UKIMWI lakini pia elimu ya kupunguza kunyanyapaa kwa waathirika na wanawatumia hawa ili kwenda kua mabalozi wazuri katika kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kupima na kutowatenga waathirika wa virusi vya UKIMWI

Sanjari na hayo Koga Mihana amesema kutakua na usajili wa vidole ambao una lengo la kuwatambua vijana ambao ni wahanga wa maambukizi ya virusi vya UKIMWI ambavyo hutumika kusajili kwa mfumo wa kidole na kupitia teknolojia hii itaenda kumtambua msajiliwa popote aendapo Tanzania kujulikana kwamba tayari amesajiliwa pia ameelezea kundi la walemavu wasio na vidole ambao wao watajisajili kwa kutumia viganja vya mikono.

Kutokana na kuwepo kwa ongezeko la maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa mikoa jirani ya Ruvuma ambayo ni Njombe,Iringa na Mbeya hivyo kuwepo kwa tamasha hili mkoa wa Ruvuma limelenga kupunguza kasi ya ukuaji wa maambukizi ya virusi vya UKIMWI ambapo mpaka kufikia mwaka 2030 Tanzania inatarajia kufikia maambukizi 0 ,unayanyapaa 0 na vifo 0.

Kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani kitaifa yanafanyika mkoa wa Ruvuma tarehe 1/12/2024 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kua ni makamu wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango.

Related Posts