Serikali yazindua vitabu vya kiada kwa Elimu ya Ualimu

Leo tarehe 25/11/2024 Serikali imezindua zoezi la ugawaji wa vitabu vya kiada kwa vyuo vya ualimu chini ambavyo vitataumika kwa walimu tarajali nchi nzima.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vitabu hivyo katika Chuo cha Ualimu Korogwe mkoani Tanga, Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ualimu nchini kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Bw. Huruma Mageni amesema kuwa leo imewekwa historia kwa nchi katika vyuo vya ualimu nchini kwa kuwa na kitabu na kitabu cha kiada.

“Leo tunazindua, uzinduzi wa vitabu vya kiada kwenye vyuo vyetu vya ualimu nchini. Kutokana na mabadiliko ya Sera na Mtaala ya mwaka 2014 toleo la 23, wote tunafahamu kwamba, Serikali ilichukua maamuzi sahihi kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi nchini kuwa na ujuzi wa kujiajiri na kuajiriwa” amesema ,Bw. Mageni

Bw. Mageni amesema, TET, ndio walifanya kazi ya kuandaa vitabu hivyo na kuongeza kuwa wanaamini sasa walimu watakakuwa kwenye mafunzo wataweza kufanya vyema mara baada ya kumaliza masomo yao ya ualimu.

Akizungumza mara baada ya kupokea vitabu hivyo , Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ualimu Korogwe ,Bi.Beatrice Nimrod, amesema kuwa anaishukuru Serikali kwa kuwapatia mtaala, mihutasari, na vitabu vya kiada vya mtaala ulioboreshwa katika ngazi ya elimu ya msingi kwa madarasa ya awali, darasa la kwanza na la tatu, na mtaala wa shule za msingi darasa la kwanza hadi la sita .

“Chuo cha Ualimu Korogwe kwa niaba ya vyuo 36 vya ualimu vya Serikali nchini, tunaahidi kusimamia matumizi ya vitabu hivyo, kwa kuhakikisha wanachuo wetu pamoja na wakufunzi wanavitumia kikamilifu katika ufundishaji na ujifunzaji”,amesema Bi.Nimrod.

Mtaala, mihtasari na vitabu iliyokabidhiwa ni kwa ajili ya tahasusi ya sayansi kwa shule zinazotumia lugha ya Kiswahili na Kiingereza kufundishia katika elimu ya msingi kwa mtaala ulioboreshwa.






Related Posts