MKAKATI: CCM IKIHITIMISHA KAMPENI KWA KISHINDO

 

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitafunga kampeni zake za uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kishindo, kwa namna ile ile kilivyozindua. Hii itadhihirika tarehe 26 Novemba 2024, wakati Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, atakapoongoza uhitimishaji huo.

Balozi Nchimbi anatarajiwa kuhitimisha kampeni hizo za CCM kwa Mkoa wa Dar es Salaam katika Uwanja wa Kwa Mnyani, Mtaa wa Kingugi, Kata ya Kiburugwa, Mbagala, Wilaya ya Temeke. Wakati huo huo, viongozi wengine, wakiwemo Wajumbe wa Kamati Kuu na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), watakuwa wakiongoza matukio kama haya katika maeneo mengine nchini.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Ndugu John Mongella, atahitimisha kampeni Mkoa wa Shinyanga, huku Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Mohamed Dimwa, akiongoza shughuli hiyo Mkoa wa Kagera.

Viongozi wengine wa CCM waliopangiwa kuhitimisha kampeni hizo siku moja kabla ya tarehe ya kupiga kura, Novemba 27, 2024, na maeneo yao ni:

• Ndugu Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa NEC – Oganaizesheni, mkoani Morogoro.
• Ndugu Amos Gabriel Makalla, Katibu wa NEC – Itikadi, Uenezi na Mafunzo, mkoani Dodoma.
• Mhe. Dkt. Isdory Phillip Mpango, Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkoani Kigoma.
• Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkoani Lindi.
• Mhe. Hemed Abdulla Suleiman, Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, mkoani Pwani.
• Mhe. Tulia Ackson, Mjumbe wa Kamati Kuu, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, mkoani Songwe.
• Mhe. Zuber Ali Maulidi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, mkoani Iringa.

Viongozi wengine waliopangiwa kuhitimisha kampeni hizo ni pamoja na:

• Ndugu Mary Pius Chatanda, Mwenyekiti wa UWT Taifa, mkoani Kilimanjaro.
• Ndugu Fadhili Maganya, Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, mkoani Manyara.
• Komredi Mohamed Ali Mohamed Kawaida, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, mkoani Rukwa.
• Ndugu Halima Mamuya, mkoani Tanga.
• Ndugu Nasir Ally Juma, mkoani Katavi.
• Ndugu Mohamed Aboud Mohamed, mkoani Ruvuma.
• Dkt. Dotto Mashaka Biteko, Mjumbe wa NEC ya CCM Taifa na Naibu Waziri Mkuu, mkoani Geita.
• Ndugu Steven Wassira, mkoani Mwanza.
• Ndugu Jackson Msome, mkoani Tabora.
• Ndugu Hussen Bashe, mkoani Mara.
• Ndugu Livingstone Lusinde, mkoani Arusha.
• Ndugu Ally Hapi, mkoani Mbeya.
• Ndugu Nape Nnauye, mkoani Mtwara.
• Ndugu Msukuma Kasheku, mkoani Simiyu.
• Ndugu Jokate Mwengelo, mkoani Njombe.
• Ndugu Mwigulu Nchemba, mkoani Singida.

CCM kuendelea kuwatumia viongozi wake na makada waandamizi katika kampeni hizi ni ishara ya jinsi chama hicho kinavyothamini fursa ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Hii ni sehemu ya demokrasia ya kuimarisha imani ya wananchi kwa CCM kama chama kinachostahili dhamana ya kuongoza.

Related Posts