CPA MAKALLA:CHADEMA HAWAKUFANYA MAANDALIZI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

*Asema waliwekeza katika kufanya maandamano, migogoro inawatafuna

Na Mwandishi Wetu

KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA Amoss Makalla amesema CHADEMA waache kulalama kuwa wagombea wake walienguliwa kwani ukweli uliopo Chama hakikuwa kimejiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Akizungumza leo Novemba 25,2024 katika Jimbo la Kinondoni Jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa mikutano yake ya kampeni ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, CPA Makalla amesema CHADEMA wamekuwa wakitumia kichaka cha wagombea kuenguliwa katika uchaguzi huo.

“Tumekuwa tukiwasikiliza wenzetu , wanapiga kelele nyingi sana kuwa wameenguliwa na wanatumia kuenguliwa kama kichaka cha kuficha madhaifu wao.Ukweli ni kwamba CHADEMA hawajujiandaa kwasababu mbili, moja baada ya Rais DK.Samia Suluhu Hassan kuruhusu mikutano ya hadhara waliamua kuwekeza katika maandamano nchi nzima.

“Wakati wanafanya maandamano CCM tulikwenda kwa wananchi kueleza kuwa mwaka huu kuna uchaguzi muhimu wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji pamoja na kutekeleza Ilani kwa ajili ya kuleta maendeleo ya wananchi,”amesema CPA Makalla.

Pia amesema CCM walimua kutoa mafunzo kwa wagombea wake kupitia wanasheria kuhusu ujazaji wa fomu za wagombeq maana walitambua umuhimu wa kujaza fomu hizo kwa usahihi.

“CCM tuliandaa wagombea wetu kwa kutumia wanasherea kupata mafunzo ya kujaza fomu za wagombea. Wenzetu hawakujiandaa na ndio maana walipokuwa wanajaza fomu mtu anaambiwa jaza jina lako anajaza mwaka wa kuzaliwa , anaambiwa jaza mwaka wa kuzaliwa anajaza namba ya simu.”

Pia amesema CHADEMA kwa sasa Wana mgororo mkubwa wa viongozi na ndio maana wameshindwa kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa na badala yake wamekuwa wakijificha katika kudai wameenguliwa.

Akizungumza kuhusu mwenendo wa kampeni za Chama hicho amesema kuwa tangu kuzindua kampeni wameendelea kufanya mikutano ya kueleza wananchi kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwani ndio msingi wa kuwa na viongozi ambao watashiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo.

Amesema kupitia kampeni za Chama hicho maelfu ya wapinzani wamejiunga na CCM na hiyo ni dalili ya kuendelea kukubalika kwa Watanzania na hawana shaka katika uchaguzi huo watashinda kwa kishindo na Wala hawajaitaji mbeleko maana yaliyofanywa na Serikali yanatosha kujenga kuaminika.

Akizungumza kuhusu kufunga kampeni kesho,CPA Makalla amesema Chama hicho kimejipanga kufunga kampeni zake kwa kishindo na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama hicho watakuwa katika mikoa yote na Katibu Mkuu wao Dk.Emmanuel Nchimbi atahitimisha kampeni katika Jimbo la Mbagala jijini Dar es Salaam.

 

Related Posts