WAHITIMU JKT WATAKIWA KUJIEPUSHA NA VIKUNDI VYA KIHALIFU

 

 

MKUU wa wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mallasa,akikagua Gwaride la Heshima kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea ‘Operesheni ya Miaka 60 ya JKT’, katika kikosi cha Jeshi cha 824 KJ Kanembwa wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

MKUU wa wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mallasa,akishuhudia kiapo cha utii cha vijana wa mafunzo ya JKT kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea ‘Operesheni ya Miaka 60 ya JKT’,katika kikosi cha Jeshi cha 824 KJ Kanembwa wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

Gwaride la Heshima la Vijana wa kujitolea likipita mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mallasa, (hayupo pichani) kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea ‘Operesheni ya Miaka 60 ya JKT’,katika kikosi cha Jeshi cha 824 KJ Kanembwa wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

Wahitimu wa JKT wakisoma risala kwa mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mallasa, (hayupo pichani) wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea ‘Operesheni ya Miaka 60 ya JKT’,katika kikosi cha Jeshi cha 824 KJ Kanembwa wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

Mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mallasa,akizungumza wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea ‘Operesheni ya Miaka 60 ya JKT’, katika kikosi cha Jeshi cha 824KJ Kanembwa wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,Mkuu wa Tawi la Logistiki na Uhandisi Makao Makuu ya Jeshi, Meja Jenerali Hawa Kodi,akizungumza wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea ‘Operesheni ya Miaka 60 ya JKT’, katika kikosi cha Jeshi cha 824KJ Kanembwa wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

Mwakilishi wa Mkuu wa JKT,Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akizungumza wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea ‘Operesheni ya Miaka 60 ya JKT’, katika kikosi cha Jeshi cha 824KJ Kanembwa wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

KAMANDA wa Kikosi Luteni Kanali Mantage Nkombe,akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea ‘Operesheni ya Miaka 60 ya JKT’, katika kikosi cha Jeshi cha 824KJ Kanembwa wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

Mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mallasa,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea ‘Operesheni ya Miaka 60 ya JKT’, katika kikosi cha Jeshi cha 824KJ Kanembwa wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

Na.Alex Sonna-KAKONKO

MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mallasa,amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya kijeshi katika kikosi cha 824 KJ Kanembwa,kutokubali kulaghaiwa kujiunga na vikundi vya kihalifu.

Kanali Mallasa,ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea ‘Operesheni ya Miaka 60 ya JKT’, katika kikosi cha Jeshi cha 824KJ Kanembwa wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

Alisema kuwa vijana wamejifunza mengi ikiwemo uzalendo,utii,ukomavu,matumizi ya silaha na mbinu mbalimbali za ulinzi na usalama.

“Mafunzo mliyoyapata ni imani yetu mtaenda kuyatumia vizuri ili lengo la Taifa kuwaanda kuwa Jeshi la Akiba na kamwe msikubali mtu awalaghai na hatimaye kujiunga na vikundi vya uhalifu”alisema Kanali Mallasa

Pia amewataka vijana hao kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yaliyo kinyume na mila na utamaduni wa Watanzania.

Alisema kuwa kupitia mafunzo hayo,Jeshi linajivunia kuwa na Jeshi la akiba lililo imara na hondari na matunda ya kazi hiyo ni kuona taifa linaendelea kuwa na amani na utulivu na kuwa na viongozi wenye kulipenda taifa na ndio msingi wa kiapo chao.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,Mkuu wa Tawi la Logistiki na Uhandisi Makao Makuu ya Jeshi, Meja Jenerali Hawa Kodi amewataka vijana hao kutumia jukwaa hilo kuwaelimisha wengine kwa vitendo kuwa wao ni wazalendo.

“Niwatake kuzingatia na kuheshimu maamuuzi yenu, kwa kufanya hivyo mtakuwa mmejitendea haki wenyewe na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na jamii mliyotoka kwa ujumla,”amesema Meja Jenerali Hawa

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa JKT, Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena, alisema Serikali inatambua na kuthamini umuhimu wa mafunzo ya JKT ndio maana imeendelea kuiongezea JKT uwezo ili vijana wengi wapate nafasi ya kujiunga katika mafunzo ya JKT.

Alisema mafunzo hayo yanaifanya Taifa linakuwa na vijana waaminifu wenye uzalendo na walio tayari kulitumikia, kulilinda na kulijenga Taifa letu la tanzania.

“Tunaishukuru Serikali chini ya uongozi Rais Samia Saluu Hassan kwa moyo wa kizalendo wa kuendeleza mafunzo haya muhimu kwa vijana wa kitanzania ili kuwa wazalendo wenye uchungu na Taifa letu.”

“Niwatake vijana mkawaelimishe wadogo na ndugu zenu umuhimu wa mafunzo ya JKT ili pindi wapatapo fursa ya kujiunga na mafunzo ya JKT wawe tayari kufanya mafunzo haya.”

Aidha, Brigedia Jenerali Mabena alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana hao kuwa nidhamu ikawe ndio silaha pekee dhidi ya jambo lolote litakalokuwa mbele yao.

“Pia yale mliyojifunza kipindi chote cha mafunzo yenu mkayaendeleze na kuyaishi huko muendako katika vikosi mtakavyopangiwa.”

Baada ya mafunzo hayo ya awali, vijana hao watapelekwa kwenye makambi mbalimbali kwa ajili ya kutumikia mkataba wa miezi 24 wakujitolea na kushiriki na kujifunza katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na kujifunza stadi za maisha kwa vitendo.

Awali Kamanda wa Kikosi Luteni Kanali Mantage Nkombe,alisema kutokana na mafunzo waliyowapatia vijana hao watakuwa chachu ya maendeleo katika jamii zao na taifa kwa ujumla na kuwakumbusha kwenda kuyaishi kwa vitendo mambo yote waliyofundishwa.

“Muendelee kuwa na nidhamu na kuepuka matumizi mabaya ya mtandao ya jamii kuepuka ushabiki wa kisiasa, vikundi viovu,ulevi, ngono matumizi ya dawa za kulevya,”amesema Luteni Kanali Nkombe.

Related Posts