TANZANI KUPUNGUZA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI, KUKUZA UTALII

Tanzania
inatarajia kuungana na nchi zaidi ya 50 duniani katika kupunguza athari za
mabadiliko ya tabianchi, yanayochangia uharibifu wa mazingira kwa ujumla na
wakati huo ikiendelea kukuza utalii.

Hayo
yameelezwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania Bw. Ernest
Mwamaja kwenye
Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa
Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) Baku, Azerbaijan,

 

Amesema
takriban asilimia 8.8 ya uharibifu wa mazingira unachangiwa na usafiiri wa anga
ambao unatumiwa zaidi katika shughuli za utalii hivyo hatua hiyo itasaidia
katika kupunguza changamoto hizo.

 

Bw.
Mwamaja amefafanua kuwa Mkutano wa COP29 umejumuisha sekta ya utalii tofauti na
ilivyokuwa miaka ya nyuma jambo ambalo litaleta faida kwa Tanzania kwani
wajumbe watakuwa wanapata wasaa wa kujadili na kupata majawabu ya athari za
mazingira.

 

Aidha,
mkurugenzi huyo amnepongeza Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo ni imeratibu
ushiriki wa mkutano huo mkubwa duniani na kuwezesha wizara, taasisi na wadau
mbalimbali kushiriki.

 

Katika
hatua nyingine, Tanzania imeshiriki mkutano wa pembezeno ili kujadili umuhimu
wa ajenda ya milima kuendelea kujadiliwa na kuingizwa rasmi kama ajenda ya COP29.

 

Mkutano
huu wa pembezeni umeandaliwa na Serikali ya Krygyzstan, Andorra na Bhutan
pamoja na Umoja wa KIRDARC.

 

Nchi
zote katika kutoa michango zimeonyesha umuhimu wa mifumo ikolojia ya milima na
namna inavyoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi. Athari hizo ni kama vile
kupotea kwa theluji, bioanuwai, kutokea kwa maporomoko ya ardhi na kukauka kwa
vyanzo vya maji. 

 

Mada
zilizozojadiliwa ni pamoja na namna Tanzania inachukua hatua kuhakikisha
ekolojia na mazingira ya milima nchini inasimamiwa na mazingira yake kutunzwa.

 

Hii
ikiwemo na kuwa na sera, sheria na mifumo ya kitaasisi inayosimamia madhubuti
utunzaji huo wa ikolojia na mazingira ya milima nchini.

 

Related Posts