Halotel yaja na mfumo wa E-SIM

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel Tanzania imekuja na Teknlojia ya E-SIM ( Embedded SIM) ,itakayochangia kuboresha huduma za mawasiliano.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 26,2024 jijini Dar es Salaam katika duka la Mlimani City, Mhandisi wa Mipango ya Vifaa wa Halotel, Leaky Wilson, amewaomba wateja wao wakiweza wabadili mfumo wa matumizi ya mawasiliano ukizingatia ya dunia inabadilika hivyo kampuni hiyo inawapa kuchagua teknolojia inayohitajika kila siku.

Amesema kwa uzinduzi huo Halotel imejiunga na harakati za kimataifa za kutumia teknolojia ya kisasa, salama na rafiki wa mazingira ambapo mfumo wa E-SIM unarahisisha kwa kuondoa kutumia kadi za SIM za kawaida badala yake ikiruhusu utendaji wa kidijitali moja kwa moja kwenye vifaa .

Ameeleza faida zinazopatikana katika teknolojia hiyo kuwa ni urahisi wa kubadilisha mtandao kutoka Halotel kwemda mitandao mingine, utendaji rahisi ambapo namba mpya zinaweza kufunguliwa kwa kutumua QR code moja kwa moja bila kutembelea duka la Halotel, usalama kwa maana ya ulinzi wa watumiaji dhidi ya kupoteza au kuibiwa kadi na utangamano.

“Inafanyakazi na vifaa vingi kama vile simu za kisasa na vifaa vinavyoweza kuvaliwa hivyo ni suluhisho kwa kila mteja wa halotel. Pia unaweza kujua kama kifaa chako kinaweza kutumia mfumo huu kwa kupiga *#06# au kutembelea duka lolote la Halotel kupata huduma hii,” amesema.

Related Posts